Saturday, March 8, 2014

YANAYOJIRI ALEXANDRIA: NILAZIMA TUUJARIBU UWANJA ...

Kocha Mkuu wa Yanga , Hans van Der Pluijm
amesema pamoja na kusafiri leo Jumamosi ,
lakini lazima waupime uwanja watakaochezea
mechi leo .
Pluijm raia wa Uholanzi amesema ni jambo la
msingi kwao kufanya mazoezi kwenye uwanja
huo , hivyo lazima .
Yanga imeanza safari leo hii asubuhi kwenda
Alexandria, mwendo wa saa mbili kutoka hapa
Cairo.
“Baada ya kufika Alexandria , lazima usiku
tutafanya mazoezi kwenye uwanja
tutakaochezea mechi.
“Kufanya hivyo kunakusaidia kuujua uwanja ,
ikiwa ni pamoja na vipimo vyake.
Ni jambo la msingi sana hata kama
hayatakuwa mazoezi ya muda mrefu,”
alisema.Yanga, kesho itashuka kwenye uwanja
huo kuwavaa mabingwa wa Afrika Al Ahly
ambao katika mechi ya kwanza waliwafunga
bao 1 -0 .

No comments:

Post a Comment