Sunday, March 30, 2014

Al Ahly yavuliwa ubingwa

MABINGWA watetezi wa soka Afrika, Al Ahly
ya Misri wametupwa nje ya Ligi ya Mabingwa
Afrika baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao
4-2 na Al Ahli Bengazi ya Libya jana.
Miamba hiyo ya Misri ilikuwa nyuma kwa bao
1-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili,
lakini walisawazisha wakati Mohamed Naguib
alipofunga katika dakika ya 40.
Lakini walikuwa nyuma tena dakika mbili
baadaye wakati Abdelrahman Fetori alipofunga
kwa penalti, na kuiacha Al Ahly ambayo iliitoa
Yanga katika raundi iliyopita, ikihitaji mabao
mawili ili isonge mbele.
Hata hivyo, mabao mengine kutoka kwa Farag
Abdel-Hafiz na Moataz El Mahdy kabla ya
dakika ya 60, yalizima matumaini ya Al Ahly
kufuzu kwa hatua ya makundi, ingawa Amr
Gamal alifunga bao la kujifariji.
Matumaini ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini
kushinda mataji matatu yalikwisha baada ya
kufungwa jumla ya mabao 3-2 na AS Vita Club
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Knowledge Musona na Morgan Gould walifunga
mabao 2-0, lakini hayakutosha kuwavusha
kwa sababu walichapwa mabao mengi katika
mechi ya kwanza.
Mabingwa mara nne wa Afrika, TP Mazembe
pia ya DRC walifuzu kwa sheria ya bao la
ugenini.
Ikiwa imefungwa mabao 2-1 katika mechi ya
kwanza, TP Mazembe ilibidi imshukuru nyota
wa Tanzania, Mbwana Samatta aliyefunga bao
katika dakika ya 66, lililotosha kuitupa nje
Sewe Sport ya Ivory Coast.
Katika mechi nyingine, Sfaxien – mabingwa wa
sasa wa Kombe la Shirikisho, walish

No comments:

Post a Comment