Klabu ya Arsenal leo imeimarisha ari yake ya
kutaka sana kushinda kombe la ligi kuu ya Premier
kutokana na bao la kipekee la Tomas Rosicky
ambalo limeinua zaidi matumaini ya Gunners dhidi
ya Tottenham.
Rosicky aliingiza bao lake dakika chache tu baada
ya mchezo kung'oa nanga.
Mchezaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor
alijaribu bahati ya kuingiza bao katika kipindi cha
kwanza wakiwa wamedhibiti mchezo ingawa
hakufua dafu.
No comments:
Post a Comment