Imeandikwa na Mwajuma Juma, Zanzibar
Imesomwa mara: 27
MAAFANDE wa Jeshi la Polisi juzi walishindwa
kufurukuta mbele ya Malindi kwa kufungwa
bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka ya
Zanzibar uliochezwa kwenye Uwanja wa
Amaan mjini Unguja.
Pambano hilo ambalo kila timu ililichukulia kwa
umuhimu wake wakati Polisi ilitaka kushinda ili
kuzidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo wakati
Malindi ikitaka kushinda kwa lengo la kujiweka
katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa
ligi hiyo.
Miamba hiyo ilionekana kushambuliana kwa
zamu katika mchezo huo kila baada ya
sekunde kuanzia kipindi cha kwanza hadi
kumalizia katika kipindi cha pili.
Malindi ambayo awali ilitangaza haina haja ya
kuwa mabingwa katika ligi hiyo, ilijipatia bao
hilo la pekee zikiwa zimebakia dakika mbili
kabla ya kwenda mapumziko, likifungwa na
Sadi Haji aliyepokea pasi safi kutoka kwa Haji
Wahaji.
Kwa matokeo hayo, Malindi imefikisha pointi
30 na kushika nafasi ya tatu wakati Polisi
inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa kuwa na
pointi 34 ikifuatiwa na Miembeni yenye pointi
31.
Saturday, March 8, 2014
LIGI KUU ZANZIBAR: MALINDI YAMTULIZA POLICE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment