Friday, March 28, 2014

Cannavaro na ronaldo style

NAHODHA wa Yanga , Nadir Haroub
‘Cannavaro ’ ana mbwembwe , baada ya
kufanikiwa kufunga penalti kwa ufundi katika
mechi dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa
Taifa, juzi , ametoa tambo zake kuwa huwa
anapiga penalti 15 kabla ya kuingia uwanjani .
Cannavaro ambaye hiyo ni penalti yake ya pili
kupiga kiufundi na kufunga baada ya kufanya
hivyo wiki mbili zilizopita katika mechi dhidi ya
Al Ahly, amejinadi kuwa ni ngumu kwake
kukosa penalti kutokana na mazoezi mengi
anayofanya ya kupiga mikwaju hiyo aliyoipa
jina la ‘Ronaldo Staili’ .
“Nimekuwa nikifanya mazoezi nikiwa na
makipa wetu kina Juma Kaseja , Ally Mustapha
‘Barthez’ na Dida (Deo Munishi), ndiyo maana
najiamini, ikitokea nikakosa itakuwa bahati
mbaya sana ,” alisema.
Mara baada ya Cannavaro kuutenga mpira
kwenye eneo la kupiga penalti, alirudi nyuma
na kuitawanya miguu yake kama anavyofanya
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, hali iliyoibua
shangwe kwa wingi .
Mwamuzi alipopuliza kipenga, Cannavaro
alirudi nyuma tena na kisha kuufuata mpira
kwa kasi, kisha kufanya kama anapiga shuti
kali, lakini akaubetua mpira huku akimchambua
kipa wa Prisons, Beno Kakolanyi ambaye
alirukia kulia na mpira ukaingia kushoto.
“Unajua ile staili nimeipa jina la ‘ Cristiano
Ronaldo Staili ’ kwa kuwa namkubali sana, si
unaonaga anavyojiandaa kupiga penalti au
faulo? Basi ndiyo kama mimi ,” alisema
Cannavaro ambaye ameteuliwa kuwa mpigaji
penalti mkuu wa timu yake .

No comments:

Post a Comment