TIMU za Soka za Jamhuri na Mafunzo juzi
zilishindwa kutambiana katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Zanzibar kwa kutoka sare ya mabao
2-2.
Mchezo huo ambao ni mwendelezo wa ligi Kuu
ya Zanzibar ulichezwa juzi kwenye uwanja wa
Amaan mjini hapa.
Waliotangulia kufunga katika mchezo huo
walikuwa ni Jamhuri ambayo ilijipatia bao lake
katika dakika ya 28 lililofungwa na mchezaji
wake Suleiman Ali Nuhu.
Mafunzo ilisawazisha katika dakika ya 56, bao
lililofungwa na Wahid Ibrahim ambaye
aliongeza la pili katika dakika ya 63.
Jamhuri ambayo tayari imeshashuka daraja
ilijitahidi kucheza kwa nguvu na kufanikiwa
kusawazisha bao hilo kunako dakika ya 73
likifungwa na Joseph Obey.
Kwa matokeo hayo, Jamhuri imefikisha pointi
nane.
Saturday, March 29, 2014
Ligi kuu Zanzibar: Mafunzo,Jamhuri hakuna mbabe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment