Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando
kwenye michezo ya mwishoni mwa juma baada ya
kufanya makosa kwenye michuano ya ligi kuu
kumwondoa kimakosa mchezaji wa Arsenal wakati
timu hiyo ilipopoteza mchezo kwa kuchapwa magoli
6-0 na Chelsea.
Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku
ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain
kushika mpira, lakini Kieran Gibbs aliondolewa
kimakosa
Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa
kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo
uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.
Hata hivyo baadae Mariner alikiri na kuomba radhi
kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa
kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa katika
mchezo huo.
Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa
kimesema kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji
kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi
husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi
Monday, March 24, 2014
REFA AWAOMBA RADHI ARSENAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment