Saturday, March 29, 2014

United yailaza Aston villa goli 4-1

MABAO mawili yaliyofungwa na straika Wayne
Rooney katika ushindi wa Manchester United
wa mabao 4 - 1
dhidi ya Aston Villa, umempa ahueni kocha wa
man United David Moyes ambaye amekuwa
akiandamwa na mabango ya kufukuzwa .
Mchezo huo , uliopigwa kwenye Uwanja wa Old
Trafford, maskani kwa Man United , wageni
ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika
dakika ya 13 Ashley Westwood kwa mpira wa
adhabu uliokwenda moja kwa moja golini .
Kuingia kwa bao hilo, liliwaamusha Man United
kwa kulisakama bao la Aston Villa na
kufanikiwa kujipatia bao dakika saba baadaye
kupitia kwa Rooney kwa kumalizia kichwa
mpira uliopigwa na kiungo Shinji Kagawa.
Wakati Villa wakipigana kusawazisha bao hilo ,
Mata alididimiza matumaini yao kwa kuongeza
bao la tatu katika dakika ya 57 , likiwa ni bao
lake la kwanza tangu ajiunga na timi hiyo
akitokea Chelsea msimu huu .
Chicharito, aliyeingia kuchukua nafasi ya
Rooney , alishindilia msumari wa mwisho katika
jeneza la Villa katika dakika 90 na kumpa
ahueni Moyes ambaye amekuwa akiandamwa
na mashabiki wakimtaka kuachia ngazi
kutokana na mwenendo wa mbaya wa timu
hiyo.

No comments:

Post a Comment