Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha
Kazi) kukamata sh. milioni 106 za klabu ya Yanga
kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi
zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake
Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.
Kupitia Msemaji wake Boniface Wambura
amesema>>’Tayari tumeanza utekelezaji wa amri
hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22
mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250
ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika
mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000′.
Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga
mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa
haki zao za kimkataba,malashi na Ndlovu
walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo
ya sh. milioni 106.
Kwa sasa wanakumbushwa wanachama wao
(klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa na vyama shiriki)kuzingatia mikataba
wanayoingia na watendaji wao wakiwemo
wachezaji, makocha na maofisa wengine.
Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate
taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi
jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka
kufanya hivyo.
Tuesday, March 25, 2014
Mahakama yaiagiza TFF kulipa Milion 106,kisa Yanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment