Katika hali ya kushangaza wenyeji timu ya Al Ahly
mpaka sasa wameshindwa kuwadhibitishia viongozi
wa Young Africans pamoja na Ubalozi wa Tanzania
nchini Misri juu ya Uwanja utakaotumika kwa ajili ya
mchezo wa marudiano Klabu Bingwa Barani Afrika
siku ya jumapili.
Sheria za mashindano ya CAF zipo wazi na
zinaelekeza timu mwenyeji wanapaswa kuwajulisha
wageni uwanja utakaotumika kwa mchezo takribani
siku 10 kabla ya mchezo, huku mpaka leo siku ya
jumatano takribani siku nne kabla ya mchezo
wakishindwa kutabanaisha mchezo utakapofanyika.
Mapema jana mchana Afisa Ubalozi wa Tanzania
nchini Misri Bw Idrisa Juma alifika makao makuu ya
Al Ahly kuweza kujua taratibu za mchezo huo lakini
hakufanikiwa kupata majibu kamili zaidi ya
kuahidiwa kufikia leo mchana kwamba watakua
wameshapata majibu juu ya ni sehemu gani mchezo
utafanyika.
Afisa Habari wa Young Africans Bw Baraka
Kizuguto leo asubuhi aliambatana na maofisa
Ubalozi mpaka makao makuu ya klabu ya Al Ahly na
kukutana na meneja Said Abdoulaziz na meneja
usalama Morgan na katika mazungumzo hayo
walisema mpaka muda huo walikuwa hawajapata
maamuzi ya serikali juu ya uwanja utakaotumika
kwa mchezo.
"Tumeomba mchezo ufanyike kati ya Uwanja wa
Cairo au mji wa Alexandria lakini Serikali imekataa
kutoa Viwanja yake pamoja na ulinzi katika mchezo
wetu kutokana na washabiki wetu kufanya vurugu
kwenye mchezo wa Super Cup dhidi ya CS Sfaxien
ya Tunisia" alisema Said.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwa zaidi ya
masaa mawili Uongozi wa Young Africans uliomba
mchezo wake ufanyike jijini Cairo kwani ndo
sehemu waliyojiandaa kwa mchezo kufuatia taarifa
ya Al Ahly walipokuja Tanzania kwenye mchezo wa
awali.
Mara baada ya mazungumzo hayo waliahidi
kuongea na waziri mwenye dhamana ya michezo
kuruhusu mchezo ufanyike jijini Cairo na kwamba
mchezo huo kama iliyoamuriwa tangu awali na
mamlaka husika ya ulinzi na usalama hautakua na
washabiki wowote kwa uwanja wowote
utakaochezewa.
Akiongea na mtandano rasmi wa klabu ya Young
Africans Kizuguto amesema wamekaa kusubiria
majibu ya Uwanja utakaotumika kwa mchezo zaidi
ya masaa 6 bila majibu huku viongozi hao wa Al
Ahly wakipigiwa simu na kutopokea.
"Tuliwaambia jiji la Cairol lina Viwanja zaidi ya 10
vyote vyenye hadhi ya kimataifa sio lazima tucheze
Cairo International, wajaribu kuomba viwanja
vingine lakini walionekana kutokua tayari na zaidi
kusisitiza watamuomba waziri wa michezo aruhusu
mchezo ufanyike Cairo bila washabiki" alisema
Kizuguto
Kutokana na mazingira hayo ya ucheleweshwaji
kutangaza sehemu utakaofanyika mchezo Ubalozi
wa Tanzania nchini Misri kupitia Balozi wake Bw
Mohamed Hamza na maafisa wake na uongozi wa
Young Africans umeendelea kufanya maandalizi
kwa njia zote kuhakikisha timu inafika salama na
kupata huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na
malazi, chakula, uwanja wa mazoezi na ulinzi kwa
kipindi chote timu itakapokuwa nchini Misri.
Msafara wa watu 30 unatarajiwa kuwasili kesho
alfajiri jijini Cairo kwa shirika la Ndege la Egypt Air
na kupokelewa Uwanja wa Ndege na Balozi Hamza,
pamoja na maafisa Ubalozi kisha kuelekea sehemu
maalumu ambayo timu ndipo itakapokua imeweka
kambi mpaka siku ya mchezo.
Wednesday, March 5, 2014
HALI TETE MISRI-AL AHLY vs YANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment