Timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara imekuwa timu
ya pili kukata tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara
msimu ujao baada ya Jumatatu ya March 24
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi
Dar mechi iliyochezwa Uwanja wa Karume 88.5
Dar es Salaam.
Ndanda imepata nafasi hiyo baada ya kuongoza
Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza ikiwa na pointi 28
na kufuatiwa na African Lyon yenye pointi 27 na
Jumatatu March 24 Lyon ilitoka sare ya bao 1-1
na Green Warriors.
Kwa hatua hiyo Ndanda inakuwa timu ya kwanza
kutoka Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kucheza
Ligi Kuu Bara ambapo awali timu ya Bandari
Mtwara ya Mtwara Mjini ndiyo ilikuwa timu ya
mwisho kucheza ligi kuu mwanzoni mwa miaka ya
2000.
Hizi ni picha za mapokezi hayo yaliyoanzia uwanja
wa Ndege wa Mtwara kisha kuelekea uwanja wa
Nangwanda Sijaona na ratiba itakamilika baadaye
kwa kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa
Makonde Beach.
Friday, March 28, 2014
hongera ndanda fc...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment