KOCHA Fred Minziro wa JKT Ruvu, amesema
kipigo cha bao 1-0 walichokipata kutoka kwa
Kagera Sugar wiki iliyopita, hakijawavunja
moyo katika mikakati yao ya kuhakikisha
wanabaki Ligi Kuu msimu ujao.
Minziro aliyeanza vizuri kibarua chake kwa
kuifunga Simba wiki mbili zilizopita kwenye
Uwanja wa Taifa, alisema baada ya kupoteza
mchezo huo, wamekamilisha maandalizi ya
mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar
utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Dar es Salaam na wana uhakika wa
ushindi.
“Inauma kupoteza mchezo, lakini bado tuna
nafasi ya kurekebisha mapungufu yetu na
kuhakikisha tunashinda mechi zilizo mbele
yetu, ikiwemo ile ya Jumapili dhidi ya Mtibwa
Sugar ili kuweka hai matumaini ya kuendelea
kusalia Ligi Kuu msimu ujao,” alisema kocha
huyo wa zamani wa Yanga.
Minziro alisema vijana wake wamempa
matumaini makubwa kutokana na jitihada
wanazozionesha kwenye mechi zilizopita,
jambo ambalo kwake ni ishara njema ya
kupata matokeo kwenye mechi zijazo.
“Tumebakiwa na michezo sita tunahitaji pointi
tisa ili kujiweka sehemu salama ili tujipange
kwa ajili ya msimu ujao ambao naamini
malengo yangu itakuwa ni kuwania ubingwa
wa Tanzania bara kutokana na kikosi
nitakacho kiunda,” alisema.
JKT Ruvu imeshacheza mechi 20 za ligi na
kubakiwa na michezo sita na inashika nafasi
ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 22.
Saturday, March 8, 2014
MINZIRO: JKT TUTARUDI MCHEZONI TU...
Location:
Ilala,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment