Friday, March 14, 2014

ANELKA ATIMULIWA BROM

Klabu hiyo iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya
Anelka kutangaza kupitia mtandao wa kijamii kuwa
anaacha kazi.
Anelka alisema kuwa anaondoka katika klabu hiyo
baada ya kukosa kutatua tofauti zilizopo kati yake
na Albion kuhusu ishara yake yenye utata ambayo
inasemekana kuwa ya kibaguzi dhidi ya wayahudi.
Mshambuluaji huyo mwenye umri wa miaka 35,
alipigwa marufuku kutocheza mechi tano na
kutozwa faini ya pauni 80,000 na shirikisho la soka
Uingereza ,kwa kufanya ishara hiyo, baada ya
kuingiza bao dhidi ya klabu ya West Ham mwezi
Disemba.
West Brom imechukua hatua ya kumfuta kazi
Anelka kutokana na ishara hiyo na pia kwa sababu
ya matamshi yake kwenye mtandao wa kijamii.
Ishara hii inapigiwa debe na msanii wa Ufaransa
Diedonne M'bala M'bala
Awali aliachishwa kazi mwa muda na Albion, wakati
klabu hiyo ilipokuwa inafanya uchunguzi wake
binafsi.
Mapema siku ya Ijumaa, Anelka alitangaza kwenye
mitandao ya kijamii kuwa anaondoka katika klabu
hiyo.
Aliandika: "kufuatia mazungumzo kati yangu na
maafisa wa klabu, kuna masharti kadhaa ambayo
wamenipa kabla ya kujiunga tena na klabu hiyo,
Masharti ambayo siwezi kuyakubali.''
Hata hivyo klabu ilisema kuwa masharti
yaliyotolewa kwa Anelka ni pamoja na kumtaka
awaombe msahama mashabiki , wadhamini na jamii
kwa ujumla kwa athari iliyotokana na ishara yake
aliyoifanya Disemba tarehe 28 na pili akubali
kutozwa faini.

No comments:

Post a Comment