UONGOZI wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) umeonyesha uzembe wa wazi kutokana
na aliyetakiwa kuwa mkuu wa msafara wa
Yanga iliyo mjini hapa anayetokea katika
shirikisho hilo , kutokuwa amewasili jijini hapa
hadi jana mchana.
Ilielezwa mjumbe aliyeteuliwa na TFF kuwa
kiongozi wa msafara alikuwa hajawasili na
kuifanya Yanga kuwa na wakati mgumu wa
mawasiliano.
Kwa kawaida , mwakilishi wa TFF ambaye ni
kiongozi wa msafara wa Yanga, alitakiwa
kufanya mawasiliano yote na Shirikisho la Soka
Afrika (Caf ) na lile la Misri (Efa ), lakini
hakuwepo.
Akizungumza, Makamu Mwenyekiti wa Yanga ,
Clement Sanga, alithibitisha kwamba kweli
kiongozi huyo wa msafara hakuwa amefika na
kazi zake nyingi zimekuwa zikifanywa na
maofisa wa ubalozi .
“Kweli hajafika na ninaweza kusema tunapata
ugumu wa mawasiliano maana Caf na
shirikisho lao linataka mtu kutoka kwenye
shirikisho letu . Sasa hayupo na ndiyo
tunaendelea kupambana tu,” alisema Sanga.
Kawaida kiongozi wa msafara hutakiwa
kuongozana na timu mwanzo hadi mwisho wa
mapambano.
Kama huyo wa TFF atakuwa amewasili leo ,
basi atakuwa amekuja Misri kuangalia mechi
kama watazamaji wengine .
Saturday, March 8, 2014
TFF YAWAPA WAKATI MGUMU YANGA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment