Thursday, March 6, 2014

ALEXANDRIA -YANGA NA AH AHLY


CHAMA cha Soka cha Egypt, EFA, kimetangaza
kuwa Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Kwanza ya
CAF CHAMPIONZ LIGI kati ya Al Ahly na Yanga
itachezwa Harras El-Hedoud Stadium Mjini
Alexandria hapo Jumapili.
Kabla ya tamko hilo kumekuwa na kutokujua wapi
pambano hilo muhimu litachezwa baada Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Misri kukataza pambano hilo
kuchezwa Mjini Cairo baada Mashabiki wa Al Ahly
wenye msimamo mkali, Ultra Ahlwy, kutamka
watahudhuria Mechi hiyo licha ya Mashabiki
kukatazwa kuingia ndani ya Uwanja.
Baada ya hapo Maafisa wa Al Ahly walianza kuhaha
kutafuta Uwanja mwingine na kuamua Mechi
ichezwe huko El Gouna Stadium kwenye Mji mdogo
wa El Gouna lakini Kocha Mkuu na Wachezaji wa Al
Ahly walipinga uamuzi huo.
Akitangaza Mechi hii kuhamishiwa huko Harras El-
Hedoud Stadium Mjini Alexandria na kuchezwa
Jumapili, Mkurugenzi wa EFA, Tharwat Suweilem,
amesema:
“Mechi itachezwa huko Alexandria na Wizara ya
Mambo ya Ndani imetutumia Barua rasmi ya
kuhakikisha usalama na sisi tumeipeleka Barua hiyo
kwa CAF na Yanga.”
Nae Kiongozi wa Al Ahly, Sayed Abdul Hafez,
anadaiwa kuzungumza na Viongozi wa Yanga
waliokuweko huko Cairo ili wakubali Gemu ichezwe
huko Alexandria baada Jana kutoa msimamo wao
kuwa hawakubali ichezwe nje ya Cairo.
Katika Mechi ya Kwanza, Al Ahly, ambao ndio
Mabingwa Watetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI,
walifungwa Bao 1-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam Wiki iliyopita kwa Bao lilofungwa na Nadir
Haroub "Cannavaro".

No comments:

Post a Comment