Monday, March 31, 2014

HAWA NDIO MAREFA WATAOCHEZESHA MECHI ZA ENGLAND MWISHO MWA WIKI HII

12.45pm Manchester City v Southampton
Referee: Chris Foy.
Assistants: M McDonough, M Wilkes.
Fourth Official: R Madley.

Aston Villa v Fulham
Referee: Michael Oliver
Assistants: J Collin, J Brooks.
Fourth Official: D Drysdale.

Cardiff City v Crystal Palace
Referee: Phil Dowd
Assistants: M Mullarkey, P Bankes.
Fourth Official: A Marriner.

Hull City v Swansea City
Referee: Howard Webb.
Assistants: D Cann, A Halliday.
Fourth Official: L Mason.

Newcastle United v Manchester United
Referee: Kevin Friend.
Assistants: J Flynn, R West.
Fourth Official: C Boyeson.

Norwich City v West Bromwich Albion
Referee: Mark Clattenburg
Assistants: G Beswick, M Scholes.
Fourth Official: C Pawson

5.30pm Chelsea v Stoke City
Referee: Lee Probert.
Assistants: S Long, R Ganfield.
Fourth Official: R East.
Sunday 6 April

1.30pm Everton v Arsenal
Referee: Martin Atkinson.
Assistants: P Kirkup, D Bryan.
Fourth Official: M Jones.

4pm West Ham United v Liverpool
Referee: Anthony Taylor.
Assistants: S Child, S Burt.
Fourth Official: C Pawson.
Monday 7 April

8pm Tottenham Hotspur v Sunderland
Referee: Lee Mason.
Assistants: S Bennett, I Hussin.
Fourth Official: M Dean.

Tottenham Boss Tim Sherwood Set to Be Sacked After Allegedly Punching a Player During a Dressing Room Bust Up Following Liverpool Defeat

Shinyanga kurudi katika ligi kuu msimu ujao

HATIMAYE wapenzi wa soka wa Mkoa wa
Shinyanga watashuhudia tena mechi za Ligi
Kuu ya soka ya Tanzania Bara msimu ujao
tangu Kahama United ambayo hapo awali
ilikuwa ikiitwa Shinyanga United, iliposhuka
daraja mwaka 2006 na hivyo kubaki wakiisikia
michuano hiyo kwenye vyombo vya habari.
Hali hiyo inatokana na matokeo ya michezo
miwili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara
Kundi C mwishoni mwa wiki yaliyotoa
mwelekeo wa timu mbili za Shinyanga za
Mwadui FC na Stand United kushinda michezo
yao na kufikisha pointi ambazo haziwezi
kufikiwa na timu nyingine za kundi hilo.
Mwadui FC ikicheza kwenye uwanja wake wa
nyumbani, iliichapa Toto African ya Mwanza
kwa bao 1-0, lililofungwa na Ibrahim Hajib
katika dakika ya 11 na bao hilo kudumu hadi
mwisho wa mchezo huo na hivyo kujikita
kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa
kujikusanyia pointi 28 kwa michezo 13.
Stand United inashika nafasi ya pili katika
msimamo wa kundi hilo baada ya kuwaadhiri
wenyeji wao, JKT Kanembwa ya Kigoma
kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini
Kigoma kwa mabao 3-2 katika mchezo
uliokuwa wa funga nikufunge na hivyo Stand
United kufikisha pointi 26.
Kwa matokeo hayo, sasa vita ya kuwania
kutinga Ligi Kuu msimu ujao imebaki kwa timu
hizo mbili za Shinyanga baada ya timu hizo
kuwa na alama ambazo haziwezi kufikiwa na
timu nyingine huku zikiwa zimebakiwa na
mchezo mmoja kila moja.
Timu ambazo zilikuwa zinazikaribia timu hizo
za JKT Kanembwa imebakiwa na pointi 20 kwa
michezo 13 nayo ikiwa imebakiwa na mchezo
mmoja, lakini hata ikishinda itafikisha pointi 23
na Toto African yenye pointi 21 imebakiwa na
mchezo mmoja ambao ikishinda itafikisha
pointi 24.
Timu nyingine zilizoshiriki kwenye Kundi C
ambazo tayari zimepoteza matumaini ya
kucheza Ligi Kuu ni mabingwa wa zamani wa
Tanzania, Pamba, Polisi ya Tabora, Polisi ya
Mara na Polisi Dodoma.

Sunday, March 30, 2014

Al Ahly yavuliwa ubingwa

MABINGWA watetezi wa soka Afrika, Al Ahly
ya Misri wametupwa nje ya Ligi ya Mabingwa
Afrika baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao
4-2 na Al Ahli Bengazi ya Libya jana.
Miamba hiyo ya Misri ilikuwa nyuma kwa bao
1-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili,
lakini walisawazisha wakati Mohamed Naguib
alipofunga katika dakika ya 40.
Lakini walikuwa nyuma tena dakika mbili
baadaye wakati Abdelrahman Fetori alipofunga
kwa penalti, na kuiacha Al Ahly ambayo iliitoa
Yanga katika raundi iliyopita, ikihitaji mabao
mawili ili isonge mbele.
Hata hivyo, mabao mengine kutoka kwa Farag
Abdel-Hafiz na Moataz El Mahdy kabla ya
dakika ya 60, yalizima matumaini ya Al Ahly
kufuzu kwa hatua ya makundi, ingawa Amr
Gamal alifunga bao la kujifariji.
Matumaini ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini
kushinda mataji matatu yalikwisha baada ya
kufungwa jumla ya mabao 3-2 na AS Vita Club
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Knowledge Musona na Morgan Gould walifunga
mabao 2-0, lakini hayakutosha kuwavusha
kwa sababu walichapwa mabao mengi katika
mechi ya kwanza.
Mabingwa mara nne wa Afrika, TP Mazembe
pia ya DRC walifuzu kwa sheria ya bao la
ugenini.
Ikiwa imefungwa mabao 2-1 katika mechi ya
kwanza, TP Mazembe ilibidi imshukuru nyota
wa Tanzania, Mbwana Samatta aliyefunga bao
katika dakika ya 66, lililotosha kuitupa nje
Sewe Sport ya Ivory Coast.
Katika mechi nyingine, Sfaxien – mabingwa wa
sasa wa Kombe la Shirikisho, walish

Yanga hoiiiiii ,Tanga

KAMA ilivyokuwa kwa Chelsea katika Ligi Kuu
ya England juzi kwa kufungwa na kutibuliwa
mbio za kuwania taji la nchi hiyo, Yanga jana
ilipata pigo kama hilo kutoka kwa Mgambo JKT
ya Tanga.
Wakati Chelsea ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa
Crystal Palace na kocha wake mbwatukaji,
Jose Mourinho akikiri mbio za ubingwa
zimekwisha, mabingwa watetezi wa Bara,
Yanga jana walichapwa mabao 2-1 na timu
hiyo ya Kabuku wilayani Handeni na kuwapa
pigo kubwa katika mbio za ubingwa.
Kwa matokeo hayo, Yanga imebakiwa na pointi
46 katika nafasi ya pili huku timu waliyokuwa
wakibanana nayo, Azam FC imefikisha pointi
53 baada ya jana kuishinda Simba kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga sasa imebakiwa na mechi nne dhidi ya
JKT Ruvu, Kagera Sugar, JKT Oljoro na Simba,
ambazo kama ikishinda zote, itafikisha 58
wakati Azam FC imebakiza mechi tatu dhidi ya
Ruvu Shooting, Mbeya City na JKT Ruvu
ambazo ikishinda zote, itafikisha pointi 62 na
kutawazwa bingwa msimu wa 2013/14.
Kwa Yanga, matokeo ya jana kwenye Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga, ni pigo kubwa
kwao kwani sasa inabidi waiombee dua mbaya
Azam FC na yenyewe ikihitaji kushinda mechi
zilizobaki ili itetee ubingwa.
Mgambo JKT ilikuwa ya kwanza kuandika bao
katika dakika ya pili tu lililofungwa na Fully
Maganga, ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Iliwachukua Yanga dakika nane za kipindi cha
pili kusawazisha kwa penalti iliyokwamishwa
wavuni na nahodha Nadir Haroub.
Bao lililoipa pigo Yanga lilifungwa kwa penalti
katika dakika ya 65 baada ya mwamuzi Alex
Mahagi wa Mwanza kuamuru pigo hilo la
adhabu kubwa kutokana na beki Kelvin
Yondani kumfanyia madhambi Malimi Busungu
akielekea kufunga.
Busungu alipiga penalti hiyo na kumfunga kipa
Juma Kaseja, na kuandika bao la pili ambalo
licha ya juhudi kubwa za Yanga kutaka
kusawazisha, hali haikuwa rahisi na hivyo
Mgambo JKT kuandika ushindi wake wa pili
mkubwa msimu huu, kwani kwenye uwanja
huo, waliifunga Simba kwa bao 1-0.

Saturday, March 29, 2014

Ligi kuu Zanzibar: Mafunzo,Jamhuri hakuna mbabe

TIMU za Soka za Jamhuri na Mafunzo juzi
zilishindwa kutambiana katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Zanzibar kwa kutoka sare ya mabao
2-2.
Mchezo huo ambao ni mwendelezo wa ligi Kuu
ya Zanzibar ulichezwa juzi kwenye uwanja wa
Amaan mjini hapa.
Waliotangulia kufunga katika mchezo huo
walikuwa ni Jamhuri ambayo ilijipatia bao lake
katika dakika ya 28 lililofungwa na mchezaji
wake Suleiman Ali Nuhu.
Mafunzo ilisawazisha katika dakika ya 56, bao
lililofungwa na Wahid Ibrahim ambaye
aliongeza la pili katika dakika ya 63.
Jamhuri ambayo tayari imeshashuka daraja
ilijitahidi kucheza kwa nguvu na kufanikiwa
kusawazisha bao hilo kunako dakika ya 73
likifungwa na Joseph Obey.
Kwa matokeo hayo, Jamhuri imefikisha pointi
nane.

Mbeya city yainyima usingizi Azam fc

KLABU ya Azam FC imeonesha wasiwasi wake
wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania
bara kwa mara ya kwanza kutokana na ugumu
wa wapinzani wao Mbeya City ambao
wanatarajia kucheza nao hivi karibuni.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye
Uwanja wa Chamazi Complex Novemba
mwaka jana, timu hizo zilitoshana nguvu kwa
kutoka sare ya mabao 3-3, na kasi hiyo ya
Mbeya City iliyopo kwenye nafasi ya tatu kwa
sasa imeonekana kuwatisha Wanalambalamba
hao na kuhofia kupoteza nafasi ya ubingwa.
Akizungumza na gazeti hili jana Katibu Mkuu
wa Azam Nassor Idrissa, alisema mchezo huo
ni mgumu hasa kulingana na ubora waliokuwa
nao wapinzani wao Mbeya City lakini
watajitahidi kushinda.
“Ni mchezo ambao tunaupa uzito wa aina yake
kwa sababu Mbeya City ni timu bora licha ya
uchanga wake ndiyo maana tunataka kwenda
Mbeya kwa tahadhari kwa sababu endapo
tutapoteza mchezo huu, hata ubingwa
unaweza kuota mbawa,” alisema Idrissa.
Idrissa alisema, pamoja na kwenda kwa
tahadhari kubwa lakini wamejiandaa
kuhakikisha wanapambana na kupata ushindi
ugenini ili kujijengea mazingira mazuri ya
kuweza kuchukua taji hilo la ubingwa wa Ligi
Kuu kwa mara ya kwanza.
“Kocha Joseph Omog ametuhakikishia
kwamba kikosi chake kipo vizuri na kinaweza
kuweka historia kwa kunyakua ubingwa wa
bara msimu huu kwakuwa hakuna
linaloshindikana kama wao walikuja kwetu
wakapata sare na sisi tunaweza kuwafunga
kwao,” alisema Idrissa.
Azam ambayo ndiyo vinara wa Ligi Kuu
Tanzania bara wakiwa na pointi 50 kabla ya
mchezo wa leo dhidi ya Simba, hawajapoteza
mchezo hata mmoja katika mechi za ligi na
endapo watashinda mchezo huo na Mbeya City
watakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa
msimu huu.

Tathmini mechi za leo ligi kuu bara

MBIO za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu
Tanzania Bara zinaendelea leo kwa timu tatu
zenye nafasi ya kutwaa taji hilo kushuka
kwenye viwanja vitatu tofauti kuwania pointi
tatu muhimu.
Mchezo wa kwanza utawakutanisha vinara wa
ligi hiyo Azam FC,ambao watakuwa uwanja wa
Taifa Dar es Salaam kupambana na Simba
mchezo ambao umevuta hisia za mashabiki
wengi wanaotaka kujua kama Simba
itakwamisha ndoto za Azam kutwaa ubingwa
msimu huu.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa
pande zote mbili hasa kwa Azam ambayo
itataka kushinda ili kuikimbia Yanga
inayoifukuzia kwa kasi kileleni licha ya tofauti
ya pointi nne zilizopo kati yao. Azam ina pointi
50 na Yanga 46.
Azam itaingia kwenye mchezo huo wa leo
ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa
mabao 2-0 iliyoupata Jumatano iliyopita dhidi
ya Mgambo JKT,kwenye uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Ni wazi kwamba itahakikisha inatumia kila aina
ya mbinu ili kupata ushindi katika mchezo huo
muhimu kwao kwa sababu inajua fika endapo
itateleza na kupoteza au kutoka sare itakuwa
imewapa nafasi nzuri wapinzani wao Yanga
kuwa na matumaini makubwa ya kutetea
ubingwa wao.
Lakini ugumu wa mchezo huo unakuja pale
ambapo Simba ambayo licha ya kuwa haina
cha kupoteza katika mchezo huo lakini
haitakubali kufungwa mara ya pili mfululizo na
Azam, kwani katika mechi ya raundi ya kwanza
ililala kwa mabao 2-1.
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema
atahakikisha leo anapanga kikosi imara
ambacho kitambana na kupata ushindi wa
pointi zote tatu ili angalau kuwapoza machungu
mashabiki wao ambao wana kumbukumbu
mbaya ya timu yao kufungwa bao 1-0 na
Coastal Union wiki iliyopita.
Kivumbi kingine kitakuwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani Tanga wakati mabingwa watetezi
Yanga watakapokuwa wakikabiliana na
Maafande wa Mgambo JKT.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na
kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa
mabao 5-0 ilioupata Jumatano iliyopita dhidi ya
Prisons na ni wazi itacheza kwa juhudi ili
kushinda mchezo huo ili kuzidi kuifukuzia
Azam iliyopo kileleni.
Kocha wa Yanga Hans Van Der Plyuijm,
amesema kila mchezo kwao ni fainali na
hawataidharau timu yoyote lengo lao likiwa
kushinda mechi zote saba zilizobaki ili kutetea
ubingwa wao.
Van Der Plyuijm alisema vijana wake
wameonesha ari kubwa ya kujituma na kupata
ushindi katika mechi tatu zilizopita hivyo hana
shaka hata katika mchezo wa leo watafanya
hivyo ili kuendelea kufukuzia ubingwa huo kwa
mara ya 25.
Mgambo JKT, ambayo haipewi nafasi ya
kushinda katika mchezo wa leo itaingia na
hasira kubwa ya kutaka kuiaibisha Yanga
baada ya kupoteza mchezo wake uliopita na
Azam FC.
Ukiacha hasira za kupoteza mchezo uliopita
kitu kingine kitakachoifanya Mgambo
kutokubali kupoteza mchezo huo ni nafasi ya
11 iliyopo kwenye msimamo ambayo ni mbaya
na huenda ikashuka daraja kama itaendelea
kupoteza mechi zake.
Mgambo ina pointi 19, na imesaliwa na
michezo mitano ili kumaliza msimu hivyo
itataka kushinda kama ilivyofanya kwa Simba
Februari 9 na kujiweka katika mazingira
mazuri ya kunusurika kushuka daraja.
Mtanange mwingine ambao leo utakuwa
unahusishwa na mbio za ubingwa ni ule
utakaowakutanisha ndugu wawili Mbeya City
na Prisons ambazo zitapambana kwenye
uwanja wa Sokoine Mbeya.
Timu hizo zitaingia katika mchezo huo zikiwa
katika hali tofauti katika mechi zao zilizopita,
Mbeya City wakitoka kuibuka na ushindi wa
mabao 2-0 ugenini dhidi ya JKT Ruvu wakati
Prisons ikikiona cha mtemakuni baada ya
kufungwa 5-0 na Yanga.
Mbeya City iliyopo kwenye kiwango bora kwa
sasa inapewa nafasi ya kushinda mchezo huo
lakini wapinzani wao Prisons siyo timu ya
kubeza licha ya kipigo hicho walichokipata
kutoka kwa Yanga.
Prisons imeonekana kuimarika zaidi kwenye
mzunguko wa pili ikiwemo kutoa vipigo kwa
timu ngumu kama Mtibwa Sugar iliyokuwa
kwenye uwanja wao wa nyumbani na kipigo
cha 6-0, ilichoipa JKT Ruvu.
Pamoja na Mbeya City kujipa matumaini ya
kushinda mchezo huo lakini isitarajie
mteremko kwani Prisons ya sasa siyo ile ya
mzunguko wa kwanza ambayo ilipata pointi 9
kwenye mechi 13 ilizocheza duru la kwanza.

United yailaza Aston villa goli 4-1

MABAO mawili yaliyofungwa na straika Wayne
Rooney katika ushindi wa Manchester United
wa mabao 4 - 1
dhidi ya Aston Villa, umempa ahueni kocha wa
man United David Moyes ambaye amekuwa
akiandamwa na mabango ya kufukuzwa .
Mchezo huo , uliopigwa kwenye Uwanja wa Old
Trafford, maskani kwa Man United , wageni
ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika
dakika ya 13 Ashley Westwood kwa mpira wa
adhabu uliokwenda moja kwa moja golini .
Kuingia kwa bao hilo, liliwaamusha Man United
kwa kulisakama bao la Aston Villa na
kufanikiwa kujipatia bao dakika saba baadaye
kupitia kwa Rooney kwa kumalizia kichwa
mpira uliopigwa na kiungo Shinji Kagawa.
Wakati Villa wakipigana kusawazisha bao hilo ,
Mata alididimiza matumaini yao kwa kuongeza
bao la tatu katika dakika ya 57 , likiwa ni bao
lake la kwanza tangu ajiunga na timi hiyo
akitokea Chelsea msimu huu .
Chicharito, aliyeingia kuchukua nafasi ya
Rooney , alishindilia msumari wa mwisho katika
jeneza la Villa katika dakika 90 na kumpa
ahueni Moyes ambaye amekuwa akiandamwa
na mashabiki wakimtaka kuachia ngazi
kutokana na mwenendo wa mbaya wa timu
hiyo.

Mashabiki waizomea ndege ya bango la "The wrong one-Moyes OUT"

Dakika chache kabla ya mchezo kati ya manchester united  na Aston villa,ndege yenye bango linalohimiza Kocha Moyes si sahihi kwa United,AONDOKE,ilikaribishwa na kelele kubwa za kuizomea kutoka kwa mashabiki waliokua uwanjani hapo. Katika maojiano kabla ya mchezo huo,Moyes alipoulizwa amelichukuliaje ilo swala la bango aliwajibu "iyo pesa ni bora wangeitumia katika Darren fletcher's charity"

Friday, March 28, 2014

Cannavaro na ronaldo style

NAHODHA wa Yanga , Nadir Haroub
‘Cannavaro ’ ana mbwembwe , baada ya
kufanikiwa kufunga penalti kwa ufundi katika
mechi dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa
Taifa, juzi , ametoa tambo zake kuwa huwa
anapiga penalti 15 kabla ya kuingia uwanjani .
Cannavaro ambaye hiyo ni penalti yake ya pili
kupiga kiufundi na kufunga baada ya kufanya
hivyo wiki mbili zilizopita katika mechi dhidi ya
Al Ahly, amejinadi kuwa ni ngumu kwake
kukosa penalti kutokana na mazoezi mengi
anayofanya ya kupiga mikwaju hiyo aliyoipa
jina la ‘Ronaldo Staili’ .
“Nimekuwa nikifanya mazoezi nikiwa na
makipa wetu kina Juma Kaseja , Ally Mustapha
‘Barthez’ na Dida (Deo Munishi), ndiyo maana
najiamini, ikitokea nikakosa itakuwa bahati
mbaya sana ,” alisema.
Mara baada ya Cannavaro kuutenga mpira
kwenye eneo la kupiga penalti, alirudi nyuma
na kuitawanya miguu yake kama anavyofanya
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, hali iliyoibua
shangwe kwa wingi .
Mwamuzi alipopuliza kipenga, Cannavaro
alirudi nyuma tena na kisha kuufuata mpira
kwa kasi, kisha kufanya kama anapiga shuti
kali, lakini akaubetua mpira huku akimchambua
kipa wa Prisons, Beno Kakolanyi ambaye
alirukia kulia na mpira ukaingia kushoto.
“Unajua ile staili nimeipa jina la ‘ Cristiano
Ronaldo Staili ’ kwa kuwa namkubali sana, si
unaonaga anavyojiandaa kupiga penalti au
faulo? Basi ndiyo kama mimi ,” alisema
Cannavaro ambaye ameteuliwa kuwa mpigaji
penalti mkuu wa timu yake .

Yanga ndani ya Tanga tayari kwa mechi ya kesho

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka ya
Tanzania Bara, Yanga wamewasili jijini Tanga
jana tayari kuvaana na Mgambo JKT katika
mchezo utakaopigwa kesho kwenye Uwanja
wa Mkwakwani.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka
Kizuguto, wamewasili salama mkoani humo, ila
alisema hana taarifa za benchi la ufundi
kuhusu hali za wachezaji katika mechi hiyo.
Hata hivyo, Yanga haina majeruhi wapya kwa
siku za karibuni kwani kikosi chake chote kiko
imara na hiyo ni muhimu hasa wakati huu
inapoifukuzia Azam FC katika kuwania ufalme
wa soka Tanzania Bara.
Mabingwa hao watetezi wako nyuma ya Azam
FC kwa pointi nne, lakini wakiwa na mchezo
mmoja mkononi, hivyo pointi tatu ni muhimu
kwao.
Yanga inaikabili Mgambo JKT ikiwa na
kumbukumbu nzuri ya kutoka kuibugiza
Tanzania Prisons kwa mabao 5-0 kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo iko
vizuri kisaikolojia.
Wapinzani wao, Mgambo JKT wametoka
kuchapwa mabao 2-0 na wapinzani wakubwa
wa Yanga, Azam FC kwenye uwanja huo wa
Mkwakwani, Jumatano wiki hii, hivyo wataingia
uwanjani kesho kama simba aliyejeruhiwa, na
hasa ikitiliwa maanani ligi inaelekea ukingoni,
na haitaki kushuka daraja.
Mgambo ni timu ambayo iko katika hatari ya
kushuka daraja kwani iko nafasi ya 11 ikiwa na
pointi 19, inaweza kutumia uwanja wake wa
nyumbani kutoka sare au ushindi hivyo Yanga
wana kibarua kizito.
Kwa upande wake, kesho Azam itavaana na
Simba yenye pointi 36 ikiwa nyuma kwa pointi
11 na ambayo imekuwa ikifanya vibaya katika
baadhi ya mechi zake.
Simba ni timu isiyotabirika inaweza ikafanya
vizuri ili wasibaki nyuma ingawa Azam pia, ni
timu inayotumia mashambulizi ya kushtukiza.
Katika mbio za kusaka ubingwa baada ya
kuvaana na Simba, bado Azam itakuwa na
kibarua kizito kwa Mbeya City, ambayo ina
kumbukumbu ya kupoteza mechi moja katika
Uwanja wa Sokoine.
Mechi nyingine zitakazochezwa kesho ni
Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons (Mbeya),
Kagera Sugar dhidi ya Ruvu Shooting (Kaitaba)
na Mtibwa Sugar itakuwa ni mwenyeji wa
Coastal Union (Manungu) wakati JKT Ruvu
itavaana na Rhino Rangers kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa Ashanti United
kukabiliana na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa
Azam Complex. Timu hizo zote ziko kwenye
hatari ya kushuka daraja, katika msimamo wa
ligi, Ashanti United ina pointi 18 wakati Oljoro
ina pointi 13. Ni tofauti ya pointi tatu.

Luis Suárez: Goodbye to England

So far this season Liverpool has made a stand
against all the top clubs in Europe. So, what exactly
is their secret? It's all too clear for the technical
staff: the answer is Luis Suárez.
Liverpool's frontman has become one of the
greatest strikers in the world, but he will not
continue at Anfield next season.
Suárez has already plumped for one of the biggest
clubs in Europe and it is not Manchester City. In
fact, the 27 year old striker will leave England
altogether.
The Uruguay attacker joined Liverpool from Ajax
when Fernando Torres joined Chelsea.

BIG MATCH


jumamosi SAA 20:30..

MASHABIKI WA MANU WAMECHOKA SASA WAAMUA KUKODI NDEGE KUMKATAA MOYES-source bbc

A group of supporters have clubbed together to pay for a light aircraft to fly over Old Trafford on Saturday, trailed by a banner that reads "Wrong One - Moyes
Out".

hongera ndanda fc...

Timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara imekuwa timu
ya pili kukata tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara
msimu ujao baada ya Jumatatu ya March 24
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi
Dar mechi iliyochezwa  Uwanja wa Karume 88.5
Dar es Salaam.
Ndanda imepata nafasi hiyo baada ya kuongoza
Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza ikiwa na pointi 28
na kufuatiwa na African Lyon yenye pointi 27 na
Jumatatu March 24 Lyon ilitoka sare ya bao 1-1
na Green Warriors.
Kwa hatua hiyo Ndanda inakuwa timu ya kwanza
kutoka Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kucheza
Ligi Kuu Bara ambapo awali timu ya Bandari
Mtwara ya Mtwara Mjini ndiyo ilikuwa timu ya
mwisho kucheza ligi kuu mwanzoni mwa miaka ya
2000.
Hizi ni picha za mapokezi hayo yaliyoanzia uwanja
wa Ndege wa Mtwara kisha kuelekea uwanja wa
Nangwanda Sijaona na ratiba itakamilika baadaye
kwa kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa
Makonde Beach.

Wednesday, March 26, 2014

Kipa wa KMKM afariki dunia

KLABU ya soka ya KMKM ya Zanzibar imepata
pigo kubwa la kuondokewa na kipa wake, Ali
Suleiman Bishoo, aliyefariki usiku wa kuamkia
jana.
Bishoo aliyekuwa kipa namba moja, alifariki
kwa kuangukiwa na mti wa aina ya mvinje
kutokana na upepo mkali uliovuma. Alifariki
dunia saa nane usiku baada ya kukutwa na
ajali akiwa na Vespa katika maeneo ya
Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.
Kwa mujibu wa Katibu wa timu hiyo, Sheha
Mohammed, kipa huyo alikutwa na mauti
wakati akitoka katika safari zake za kawaida.
“Tumepata pigo kubwa, lakini kazi ya Mungu
haina makosa…sisi tulimpenda, lakini yeye
amempenda zaidi,” alisema Katibu huyo.
Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja na
ulitarajiwa kuzikwa jana kijijini kwao Cheju
Mkoa wa Kusini Unguja.
Bishoo alikuwa ni miongoni mwa makipa
waliochaguliwa katika timu ya Taifa ya
Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, lakini alizuiwa na
KMKM, hivyo kufungiwa kutocheza soka kwa
msimu mzima wa ligi na ZFA Taifa.
Awali, mabaharia hao wa KMKM juzi
walijiweka katika mazingira mazuri katika
msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar baada ya
kufikisha pointi 36 kutokana na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri.
Jamhuri katika mchezo huo watapaswa
kujilaumu kutokana na kukosa mabao mengi
ya wazi pamoja na penalti iliyopigwa na
Suleiman Ali Nuhu katika dakika ya 82.
Mabao ya KMKM yaliyowawezesha kuondoka
na ushindi huo yalifungwa na Mudriki Muhibu,
moja akilifunga katika dakika ya 14 na la pili
dakika ya 44.
KMKM sasa inashika nafasi ya pili, huku Polisi
ikiongoza kwa pointi 37, na kubakiwa na
michezo miwili, ambayo kama Polisi ikipoteza
mmoja na KMKM kushinda yote, basi
itatawazwa bingwa.

Prisons wachezea mkono!! bila majibu... Jangwani kicheko

YANGA SC leo imefanya mauaji baada ya
kuishushia kipondo cha bao 5- 0 Tanzania
Prisons kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara
iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam . Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani
na
Emmanuel Okwi dakika ya 20, Mrisho Ngassa
dakika ya 37, Hamis Kiiza aliyetupia mawili
dakika ya 68 na 88 pamoja na Nadir Haroub
'Cannavaro ' dakika ya 78.

Tuesday, March 25, 2014

Mahakama yaiagiza TFF kulipa Milion 106,kisa Yanga.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha
Kazi) kukamata sh. milioni 106 za klabu ya Yanga
kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi
zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake
Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.
Kupitia Msemaji wake Boniface Wambura
amesema>>’Tayari tumeanza utekelezaji wa amri
hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22
mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250
ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika
mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000′.
Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga
mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa
haki zao za kimkataba,malashi na Ndlovu
walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo
ya sh. milioni 106.
Kwa sasa wanakumbushwa wanachama wao
(klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa na vyama shiriki)kuzingatia mikataba
wanayoingia na watendaji wao wakiwemo
wachezaji, makocha na maofisa wengine.
Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate
taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi
jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka
kufanya hivyo.

Pep Guardiola TAYARI ASHATANGAZWA KUTWAAA UBINGWA

Bayern Munich wametwa taji la
Bundesliga kwa kuweka historia ya kufanya hivyo baada ya michezo 27 tu. Hiyo inafuatiaushindi wao wa 3-1 dhidi ya Berlin!

Hili ni taji lao la 24 la Bundesliga, wakicheza mechi 52 bila kufungwa na ushindi wa leo ni wa
19 mfululizo.

rufaa ya real madrid dhidi ya sergio ramos imekataliwa na kuonekana ni ya halali hivyo atatumikia adhabu chake

ukicheza na barca jiandae kucheza name wachezaji kumi ndani

by:
sio Mimi ni mourinho joseee

RATIBA YA SOKA LEO JUMATANO 26th march 2014: *Barclays Premier League 10:45 PM - West Ham United vs Hull City 11:00 PM - Liverpool vs Sunderland *Spanish Primera División 10:00 PM - Barcelona vs Celta Vigo 10:00 PM - Rayo Vallecano vs Osasuna 27th march 2014 12:00 AM - Atletico Madrid vs Granada 12:00 AM - Sevilla FC vs Real Madrid *Italian Serie A 10:45 PM - Atalanta vs Livorno 10:45 PM - Cagliari vs Hellas Verona 10:45 PM - Catania vs Napoli 10:45 PM - Chievo Verona vs Bologna 10:45 PM - Fiorentina vs AC Milan 10:45 PM - Genoa vs Lazio 10:45 PM - Juventus vs Parma 10:45 PM - Sassuolo vs Sampdoria *German Bundesliga 10:00 PM - Eintracht Frankfurt vs Borussia Monchengladbach 10:00 PM - FC Augsburg vs Bayer Leverkusen 10:00 PM - Hamburg SV vs SC Freiburg 10:00 PM - Nurnberg vs VfB Stuttgart 10:00 PM - TSG Hoffenheim vs Hannover 96 *French Coupe de France 8:45 PM - Cannes vs Guingamp 10:55 PM - AS Monaco vs Lens # EAT

Kuelekea manchester derby usiku wa leo

Manchester United ? ? Manchester City
-Wayne "WAZZA" Rooney ndiye anayeongoza kwa
magoli kwenye derby hii. Magoli 11.
-Michezo 4 iliyopita Manchester United ameshinda 1
na kupoteza 3.
-Manchester United wanahitaji ushindi kwenye
mchezo huu ili wajiweke nafasi nzuri ya kushiriki
UEFA msimu ujao.
-Manchester City wanahitaji ushindi kwenye mechi ya
leo ili wawe kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.

Monday, March 24, 2014

Ronaldo: Marefa wanatuonea

Mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo amesema
kwamba marefa hawawatendei haki kila
wanapokutana na wapinzani wao wa jadi,
Barcelona.
Ametoa kauli hiyo baada ya Real Madrid kufungwa
4-3 na mabingwa hao wa Hispania kwenye mechi
ya kukata na shoka Jumapili hii.
Ronaldo anasema kwamba haielezeki jinsi maamuzi
mabaya yanavyotolewa na waamuzi kwenye mechi
baina yao, ambapo Jumapili hii Real Madrid
walikuwa wamejiamini sana kwamba wangeshinda
kutokana na rekodi yao ya hivi karibuni.
Katika mechi hiyo, mwamuzi Alberto Undiano
Mallenco alitoa penati tatu lakini pia alimyoa nje kwa
kadi nyekundu mchezaji Sergio Ramos wa Real
Madrid katika uwanja wao wa nyumbani wa
Santiago Bernabeu.
Lionel Messi alitupia mabao mawili kwa penati tata
kama sehemu ya hat-trick yake, ambapo Barca
walitoka kusinzia 3-2 na kuwalaza Madrid 4-3 na
kufufua upya ndoto zao za ubingwa.
“Ni ngumu sana kwa sababu watu wengi
hawakutaka tushinde kwa vile kwa kufanya hivyo
Barcelona wangekuwa wametupwa nje ya
kinyang’anyiro cha ubingwa wa Hispania. Labda
hawataki tuchukue kombe hili,” alisema Ronaldo.
Mreno huyo mwenyewe alifunga bao kwa penati tata
pia baada ya Dani Alves kumwangusha nje ya boksi
la penati. Ramos alipotolewa nje kwa kumpiga
kwanja Neymar kwenye mstari wa boksi, wageni
waliona kwamba wakati wao wa kujidai ulifika, na
kweli Messi akasawazisha kwa penati.
Barca ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika
dakika ya saba kupitia kwa Andres Iniesta lakini
likasawazishwa na Karim Benzema dakika ya 24
kabla Mfaransa huyo huyo hajaongeza jingine
dakika ya 24.
Hata hivyo, penati aliyotumbukiza kwenye kwamba
Messi ilikuja dakika ya 42 kabla ya hasimu wake,
Ronaldo kufunga yake dakika ya 55. Dakika 10
baadaye Messi alifunga tena kwa penati dakika ya
65 kabla ya kufumania nyavu dakika sita kabla ya
mechi kumalizika.
“Tunasikitika sana kwa matokeo haya, kwa sababu
ukweli ni kwamba tulitakiwa tushinde sisi,”
akasema Ronaldo ambaye wakati wa mechi alifika
mahali akamfuata mwamuzi kumlalamikia.
Matokeo hayo yanawafanya Atletico Madrid
kuongoza ligi kwa kufikisha pointi 70 sawa na Real,
huku wakifuatiwa na Barca wenye pointi moja
pungufu na Athletic Bilbao wenye pointi 55.

Singano(messi) akokotwa polisi

WINGA machachari wa Simba, Ramadhan
Singano juzi alilazimika kupelekwa kwenye
Kituo cha Polisi cha Chang’ombe katika Mkoa
wa Kipolisi wa Temeke, na Katibu Mkuu wa
timu hiyo, Ezekiel Kamwaga.
Hiyo ilitokana na mchezaji huyo kuvunja kioo
cha moja ya mlango wa kuelekea kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo uwanjani hapo
kwa kukipiga teke, muda mfupi baada ya
mchezo kati yao na Coastal Union ya Tanga
kumalizika wakiwa wamelala kwa bao 1-0.
Kutokana na kitendo hicho cha utovu wa
nidhamu na uharibifu wa mali ya umma, askari
Polisi waliokuwepo uwanjani wakilinda
usalama, walipanga kuondoka na mchezaji
kumpeleka kituoni, lakini viongozi wa timu hiyo
waliingilia kati na kuamua kumpeleka wao ili
akatoe maelezo.
“Katibu wetu Kamwaga (Ezekiel) ndiye
aliyempeleka Singano, kituo cha Polisi ili
akaandike maelezo kuhusu uharibifu
alioufanya. Ni kweli askari wa Jeshi la Polisi
walipanga kuondoka naye, lakini tulizungumza
nao hasa kwa kuzingatia jina alilokuwa nalo
mchezaji,” alisema Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Simba, Saidi Pamba.
Pamba alisema baada ya kuandikisha maelezo,
mchezaji huyo ambaye pia anaichezea Taifa
Stars, aliachiwa huru huku wakisubiri Jeshi
hilo lifanye kazi yake kwa kushirikiana na
mamlaka husika kwa maana ya Shirikisho la
Soka (TFF) na Uwanja wa Taifa kufahamu
gharama ya uharibifu alioufanya winga huyo.
“Tunasubiri ripoti ya Polisi iweze kutoa majibu
baada ya kumaliza uchunguzi endapo
atatakiwa kulipa faini hiyo, atalazimika
kulimaliza mchezaji mwenyewe na kama
atakuwa hana Simba itamlipia, lakini kwa
masharti ya kumkata kwenye mshahara
wake,” alisema Pamba.
Katika mchezo huo, Singano alipoteza nafasi
nyingi za kufunga mabao ikiwemo ile ya dakika
ya mwisho aliyoipata na kushindwa kuisaidia
timu yake kuepuka na kipigo katika mchezo
huo.
Kutokana na matokeo hayo yaliyowakera
mashabiki wa timu hiyo, Pamba alisema jana
Kamati ya Utendaji pamoja na ile ya Ufundi
zilitarajiwa kuwa na mkutano kujadili sababu
ya timu hiyo kufanya vibaya na namna gani ya
kushinda mechi nne zilizosalia kabla msimu
huu haujamalizika.
Katika msimamo wa ligi, Simba inashika nafasi
ya tatu ikiwa na pointi 36, pointi sita nyuma ya
wanaoshika nafasi ya tatu Mbeya City, pointi
saba nyuma ya Yanga na pointi 11 nyuma ya
vinara.

Mkwasa akiri mechi dhidi ya prisons itakua ngumu

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka
Bara, Yanga wamesema pambano dhidi ya
Tanzania Prisons sio mechi rahisi kama
ambavyo wengi hudhani, hivyo wana kazi ya
kujipanga ili kuchukua pointi tatu muhimu.
Yanga wamerejea Dar es Salaam juzi
wakitokea Tabora walikokuwa na mechi dhidi
ya Rhino Rangers ambako walipata ushindi wa
mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na jana jioni
ilitarajiwa kuanza kujifua kwenye uwanja wake
tayari kwa mechi ya kesho.
Mabingwa hao wa Bara wanatarajiwa kushuka
dimbani kesho kuvaana na maafande hao wa
Magereza kutoka Mbeya katika mechi
itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha
Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa
alisema katika kuelekea mwishoni mwa
msimu, kila timu hujipanga kufanya vizuri ili
kuendelea kubaki katika nafasi nzuri, hivyo
anafikiri mechi hiyo huenda ikawa ngumu.
“Tunaelekea mwishoni mwa msimu, upinzani
utakuwa ni mkali kwa sababu kila timu
inajipanga kubaki katika nafasi nzuri, na wakati
huo, tusipokuwa makini mchezo utakuwa ni
mgumu,” alisema Mkwasa ambaye alifundisha
na kuipa ubingwa wa Tanzania, Prisons
mwaka 2000.
Mkwasa alisema wachezaji wake wote wako
salama hivyo wataendelea na mazoezi mepesi
jana na leo tayari kwa mchuano huo wakiwa na
lengo la kufanya vizuri ili kuchukua tena
ubingwa.
Kuhusu kipa wao namba moja, Deogratius
Munishi, Mkwasa alisema hajapata uhakika
kama atakuwepo mpaka apate maelezo ya
daktari wao.
Kwa upande wake, daktari wa Yanga, Juma
Sufiani alisema Munishi anaendelea na
matibabu na hajawasiliana naye kuona kama
amepata nafuu kwa vile alikuwa safarini.
Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
Yanga iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi
43 nyuma ya Azam yenye pointi 47, wakati
Tanzania Prisons iko katika nafasi ya 10 ikiwa
na pointi 22.
Hata hivyo, Yanga iko nyuma mchezo mmoja
na Azam FC kesho itakuwa Tanga kuikabili
Mgambo JKT.

REFA AWAOMBA RADHI ARSENAL

Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando
kwenye michezo ya mwishoni mwa juma baada ya
kufanya makosa kwenye michuano ya ligi kuu
kumwondoa kimakosa mchezaji wa Arsenal wakati
timu hiyo ilipopoteza mchezo kwa kuchapwa magoli
6-0 na Chelsea.
Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku
ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain
kushika mpira, lakini Kieran Gibbs aliondolewa
kimakosa
Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa
kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo
uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.
Hata hivyo baadae Mariner alikiri na kuomba radhi
kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa
kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa katika
mchezo huo.
Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa
kimesema kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji
kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi
husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi

FIFA U17 Women’s World Cup | RESULTS

Colombia 1 - 3 China PR
Nigeria 3 - 0 Mexico
Japan 3 - 0 New Zealand
Venezuela 1 - 0 Italy
Zambia 2 - 1 Costa Rica
Canada 2 - 1 Ghana
Korea DPR 4 - 3 Germany

Sunday, March 23, 2014

AZAM FC MAMBO SAFI....SIMBA HOI...

AZAM FC imezidi kutakata kileleni mwa
msimamo wa Ligi Kuu ya soka ya Tanzania
Bara kwa kupata ushindi dhidi ya Oljoro JKT
wakati Simba hali yake inazidi kwenda mrama
baada ya kuzamishwa nyumbani na Coastal
Union ya Tanga.
Kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya maafande
hao wa Arusha, Azam FC imefikisha pointi 47
na kuiacha Yanga nyuma kwa pointi nne,
ingawa mabingwa hao watetezi wana mchezo
mmoja mkononi.
Kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
Simba ilizidi kujiweka katika wakati mgumu
msimu huu na huenda ikakosa hata nafasi ya
tatu kufuatia kipigo cha bao 1-0 ilichokipata
kutoka kwa Coastal Union.
Vijana wa Msimbazi waliuanza mchezo huo
kwa kasi na kupoteza nafasi nyingi kipindi cha
kwanza kupitia kwa washambuliaji Amis
Tambwe, Ramadhani Singano, Haruna
Chanongo na kiungo wake Jonas Mkude.
‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union iliwabidi
kusubiri hadi dakika ya 45 kujipatia bao pekee
lililofungwa na Hamadi Juma aliyewalamba
chenga walinzi wa Simba, Donald Mosoti na
Joseph Owino kisha kupiga shuti lililompita
makwapani kipa Ivo Mapunda na kutinga
wavuni.
Katikati ya kipindi cha kwanza, Kocha Mkuu
wa Simba, Zdravko Logarusic alimtoa nje
kiungo mkongwe Henry Joseph kutokana na
kutoridhishwa na kiwango chake na
kumwingiza Said Ndemla.
Kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko kwa
kumtoa beki wa kushoto Omari Salum na
kumwingiza William Lucian aliyeipa uhai timu
hiyo kwa kupiga krosi nyingi kwenye lango la
wapinzani wao, lakini washambuliaji
walishindwa namna ya kumfunga kipa
chipukizi wa Coastal Union, Fikiri Selemani.
Coastal Union ambayo iliwachezesha
wachezaji wengi wa kikosi cha vijana,
walionekana kutulia na kutengeneza
mashambulizi yao kwa umakini kupitia kwa
Daniel Lyanga na Kenneth Masumbuko, ambao
walionekana kuisumbua ngome ya Simba mara
kwa mara, lakini hakufunga bao jingine.
Dakika tano za mwisho Simba ilionekana
kupania kusawazisha bao hilo baada ya
kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la
Coastal Union, lakini kipa Seleman aliibuka
nyota wa mchezo baada ya kumdhibiti Singano
kufunga bao katika dakika ya mwisho ya
mchezo.
Baada ya filimbi ya mwisho, Singano alikwenda
kuvunja kioo cha mlango wa kuingilia kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo, hivyo Jeshi la
Polisi kulazimika kumsubiri ili kumpeleka
kituoni kwa maelezo zaidi.
Kwa matokeo hayo, Simba imebaki katika
nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake 36, pointi
sita nyuma ya wanaoshika nafasi ya tatu
Mbeya City, pointi saba nyuma ya Yanga na
pointi 11 nyuma ya vinara.
Kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
wenyeji Azam FC walijipatia bao la ushindi
katika dakika ya 71 lililofungwa na John Bocco
kutokana na pasi ya chipukizi Kelvin Friday.
Katika mechi nyingine, Ruvu Shooting iliichapa
Ashanti United kwa mabao 2-0 kwenye
Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabao hayo yalifungwa na Elias Maguli dakika
za sita na 63.
Ruvu imefikisha pointi 31 baada ya mechi 22
katika nafasi ya sita wakati Ashanti ni ya 12 na
pointi zake 19. Jijini Tanga, wenyeji Mgambo
JKT walilazimishwa sare ya bao 1-1 na
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM
Mkwakwani.
Mgambo imebaki nafasi ya 11 ikiwa na pointi
19 kwa mechi 21, wakati Mtibwa Sugar inabaki
nafasi ya nane kwa pointi zake 27 baada ya
mechi 22.
Ligi hiyo itaendelea keshokutwa Jumatano kwa
mechi kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons
kwenye Uwanja wa Taifa na Mgambo JKT
dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa
Mkwakwani.

Matokeo ya Real Madrid vs Barcelona march 23 2014

Friday, March 21, 2014

hizi ndio mechi atazokosa robin van persie

HIZ NDIO MECHI AMBAZO RVP
ATAZIKOSA KUTOKANA NA KUUMIA

aliumia dhid ya mechi ya
Olympiacos baada ya hat trick

Mar 23: West Ham (A)
Mar 25: Man City (H)
Mar 29: Aston Villa (H)
Apr 1: Bayern Munich (H)
Apr 5: Newcastle (A)
Apr 9: Bayern Munich (A)
Apr 20: Everton (A)
Apr 26: Norwich (H)

JE UNATAKA KUJUA ZAWADI ALIYOPEWA ARSENAL NA CLUB YAKE KATIKA MECHI YA 1000 KESHO DHIDI YA CHELSEA

RATIBA ROBO FAINALI UEFA HII HAPA

Barcelona vs Atletico Madrid
Real Madrid vs Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain vs Chelsea
Manchester United vs Bayern Munich

Ni kweli man u mtelemko kias hiki?????

Sunday, March 16, 2014

ARSENAL YAICHAPA SPURS GOLI 1

Klabu ya Arsenal leo imeimarisha ari yake ya
kutaka sana kushinda kombe la ligi kuu ya Premier
kutokana na bao la kipekee la Tomas Rosicky
ambalo limeinua zaidi matumaini ya Gunners dhidi
ya Tottenham.
Rosicky aliingiza bao lake dakika chache tu baada
ya mchezo kung'oa nanga.
Mchezaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor
alijaribu bahati ya kuingiza bao katika kipindi cha
kwanza wakiwa wamedhibiti mchezo ingawa
hakufua dafu.

AJALI BASI LA YANGA

Bus la timu ya Young Africans lililokuwa limebeba
wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi
limepata ajali eneo na Mikese Mizani baada ya
Mabus yaliyokua yakitanua kuelekea mikoa ya
bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia
kwenye mtaro.

Friday, March 14, 2014

ANELKA ATIMULIWA BROM

Klabu hiyo iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya
Anelka kutangaza kupitia mtandao wa kijamii kuwa
anaacha kazi.
Anelka alisema kuwa anaondoka katika klabu hiyo
baada ya kukosa kutatua tofauti zilizopo kati yake
na Albion kuhusu ishara yake yenye utata ambayo
inasemekana kuwa ya kibaguzi dhidi ya wayahudi.
Mshambuluaji huyo mwenye umri wa miaka 35,
alipigwa marufuku kutocheza mechi tano na
kutozwa faini ya pauni 80,000 na shirikisho la soka
Uingereza ,kwa kufanya ishara hiyo, baada ya
kuingiza bao dhidi ya klabu ya West Ham mwezi
Disemba.
West Brom imechukua hatua ya kumfuta kazi
Anelka kutokana na ishara hiyo na pia kwa sababu
ya matamshi yake kwenye mtandao wa kijamii.
Ishara hii inapigiwa debe na msanii wa Ufaransa
Diedonne M'bala M'bala
Awali aliachishwa kazi mwa muda na Albion, wakati
klabu hiyo ilipokuwa inafanya uchunguzi wake
binafsi.
Mapema siku ya Ijumaa, Anelka alitangaza kwenye
mitandao ya kijamii kuwa anaondoka katika klabu
hiyo.
Aliandika: "kufuatia mazungumzo kati yangu na
maafisa wa klabu, kuna masharti kadhaa ambayo
wamenipa kabla ya kujiunga tena na klabu hiyo,
Masharti ambayo siwezi kuyakubali.''
Hata hivyo klabu ilisema kuwa masharti
yaliyotolewa kwa Anelka ni pamoja na kumtaka
awaombe msahama mashabiki , wadhamini na jamii
kwa ujumla kwa athari iliyotokana na ishara yake
aliyoifanya Disemba tarehe 28 na pili akubali
kutozwa faini.

Tuesday, March 11, 2014

Matokeo ya mechi za jana

MABADILIKO YA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM

LIGI HIYO ITAMALIZIKA APRIL 19 BADALA YA APRIL
27 mwaka huu.
Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi
26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati
Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo huo ni
Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili;
Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa Sugar
itacheza na Yanga (Jamhuri).
Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu
Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika
Kagera Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa
mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba),
JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex),
Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi).
Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa),
Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani),
Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini)
Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi 29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa
mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam Complex)
wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine),
Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba),
Mtibwa vs Coastal (Manungu),
JKT Ruvu vs Rhino (Azam Complex),
Azam vs Simba (Taifa),
Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa
Kagera vs Simba (Kaitaba),
Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex).
Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo
(Mkwakwani),
Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid),
Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi),
Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini)
Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa
Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini),
Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani),
Prisons vs Rhino (Sokoine).
Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera
(Mkwakwani),
Simba vs Ashanti (Taifa),
Mbeya City vs Azam (Sokoine)
Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs
Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi),
Mbeya City vs Mgambo (Sokoine),
Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro),
JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex),
Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid),
Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba
(Taifa).

Saturday, March 8, 2014

PICHA 23 ZA CHRISTIANO RONALDO WA NJE YA UWANJA

Picha zinamuonesha CR7 akiwa na baadhi ya wasichana aliowai kuwa nao katika mahusiano nao kipindi cha nyuma pamoja na ya mchumba wake wasasa Irana Shyke. Pia magari anayomilika pamoja na muonekano we maeneo tofauti ndani ya nyumba yake.