Young Africans imeendeleza wimbi lake la ushindi
katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara hatua ya
lala salama baada ya kuichapa timu ya Wakata
miwa Kagera Sugar kutoka mjini Bukoba kwa
mabao 2-1 mchezo uliofanyika jioni ya leo kwenye
dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao
5-1 mwishoni mwa wiki dhidi ya maafande wa jeshi
la Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu, Kikosi cha Young
Africans kiliingia uwanjani kuhakikisha kinapata
pointi 3 jambo ambalo vijana walifanikiwa.
Kwa matokeo ya leo ya 2-1 dhidi ya Kagera Sugar
yanaipelekea Young Africans kufikisha pointi 52
ikiwa ni pointi moja nyuma ya Azam FC yenye pointi
53 na wauza ramba ramba wakiwa nyuma kwa
mchezo mmoja kufuatia mechi yao kuahirishwa leo
kutokana na mvua zilizopelekea uwanja wa
mabatini kujaa maji.
Hamisi Kizza aliipatia Young Africans bao la kwanza
dakika ya tatu ya mchezo akiunganisha krosi safi
ya winga Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa
Kagera Sugar na kumimina krosi hiyo iliyomkuta
mfungaji aliyeukwamisha mpira wavuni na kufikisha
idadi ya mabao 12 kwenye michezo wa Ligi Kuu
msimu huu.
Young Africans iliendelea kulishambulia lango la
Kagera Sugar kupitia kwa Didier Kavumbagu,
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa na Hamisi Kizza lakin
kutokua makini kwa wachezaji hao kulifanya
waopoteze nafasi nyingi za wazi.
Dakika ya 34 ya mchezo, mshambuliaji wa
kimataifa kutoka nchini Burundi Didier Kavumbagu
aliwainua washabiki wa Young Africans vitini baada
ya kuipatia timu yake bao la pili baada ya jitihada
zake binafasi kufuatia kuwazidi ujanja walinzi wa
Kagera Sugar na kuukwamisha mpira wavuni na
kufikisha idadi ya mabao 11 kwenye VPL.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza
zinamalizika, Young Africans 2 - 0 Kagera Sugar.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya
mabadiliko na kusaka mabao ya mapema, lakini
uimara wa mlinda mlango wa Yanga SC Deo Munish
"Dida" ulikua kikwazo kwa washambuliaji wa
Kagera Sugar na kuokoa michomo zaidi ya mitatu
ya hatari langoni mwake.
Makosa ya mlinzi wa Young Africans Oscar Joshua
yaliipatia Kagera Sugar bao la kwanza dakika ya 63
baada ya mpira wa kichwa aliomrudishia golikipa
wake Dida kunaswa na Daud Jumanne ambaye
aliukwamisha wavuni na kuhesabu bao la kwanza
kwa timu yake.
Young Africans iliendelea kulishambulia lango la
Kagera Sugar bila mafanikio kipindi cha pili kufuatia
washambuliaji wake kutokua makini katika
umaliziaji na kukuta mipira ikiokoloewa na golikipa
wa Agathony Anthony na mingine kuwa kona
ambazo hazikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young
Africans 2- 1 Kagera Sugar.
Mara baada ya mchezo wa leo kikosi cha Young
Africans kesho kitaendelea na mazoezi jioni
kujiandaa na safari ya jijini Arusha kwenda kuwavaa
JKT Oljoro mwishoni mwa wiki kabla ya kurejea Dar
es salaam kumalizia mchezo wa mwisho dhidi ya
watani wa jadi Simba Sc.
Young Africans: 1.Deo Munish "Dida" 2. Jumva
Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub
"Cannavaro", 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo,
7.Saimon Msuva, 8.Hassan Dilunga, 9.Didier
Kavumbagu, 10.Mrisho Ngasa/Hussein Javu,
11.Hamisi Kizza/Nizar Khalfani
Wednesday, April 9, 2014
Yanga yachapa mtibwa bao 2-1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment