KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema
ni matumaini yake kuwa anaenda kumaliza kiu
ya kukosa ushindi kwa muda mrefu kwa
kutwaa Kombe la FA.
Wenger alisema ikiwa ni mwaka wa tisa sasa
bila ya kuchukua kombe, anaona kuwa msimu
huu ni muda mwafaka wa kuchukua kombe
hilo.
Alisema ana imani kuwa katika mchezo wake
wa leo wa nusu fainali dhidi ya Wigan, ushindi
ndio kupaumbele kikubwa na amekuwa
akisisitiza kwa kiasi kikubwa suala zima la
ushindi katika ligi hiyo.
Baada ya kutolewa kwenye kinyang'anyiro cha
kuwania Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa nia
yake kubwa ni kuhakikisha kuwa anachukua
moja kati ya mataji ya ndani.
“Ligi ya Mabingwa ndio ilikuwa kila kitu kwetu
na hadi sasa bado naumia kukosa ubingwa
huo, lakini kwa sasa mimi pamoja na timu
yangu nzima tunahamishia harakati zetu za
ushindi kwa michuano ya ndani,” alisema
Wenger ambaye amekuwapo Arsenal kwa
miaka 18 sasa.
“Najua kila mmoja aliyepo kwenye Ligi ya
England anakuwa na shauku ya kuhakikisha
kuwa anashinda na kuibuka na ushindi na ndio
azma yetu kwa sasa,” alisema Wenger.
“Usishangae kuona kwa miaka tisa sina kombe
lolote, sasa ndio ujue ni kwa kiasi gani
ninakuwa na hasira ya ushindi kwa sasa na
nipo tayari kuchukua Kombe la FA,” alisema
Wenger.
Alisema nia yao kwa sasa ni kushinda
mashindano na hasa ikizingatiwa kuwa
hawana mchakato wowote wa kuwania Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Aliongeza kuwa wanarejea Wembley wakiwa
wamejikamilisha na kusahau yote yalyotokea
kwenye Kombe la mwisho la FA, Arsenal
walichukua mwaka 2005 baada ya kuitoa
Manchester United katika fainali.
Friday, April 11, 2014
WENGER: Nina hasira na ushindi, sasa naenda kuchukua FA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment