WACHEZAJI watatu wa Tanzania wanaocheza
soka la kulipwa nje watakosa katika mechi ya
kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Burundi
itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Boniface Wambura alisema wachezaji
hao ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu
wanaocheza TP Mazembe ya Congo na Mwinyi
Kazimoto anayekipiga Qatar.
“Tuliandika barua kuwaomba wachezaji hao,
lakini tunaona kuwa kama watakosa mechi hii
basi watashiriki katika mechi ya mchujo
kuwania Kombe la Mataifa la Afrika, lakini
katika mechi ijayo watacheza wale wa ndani,”
alisema Wambura.
Alisema mchezo huo wa Jumamosi utakuwa ni
sehemu ya kusherehekea miaka 50 ya
Muungano.
Katika mechi hiyo itashuhudiwa na kocha
mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatus Nooij
ambaye anatarajiwa kutua nchini Ijumaa, na
baada ya mechi atatambulishwa rasmi na Rais
wa TFF, Jamal Malinzi.
Nooij ni kocha wa St. George ya Ethiopia na
tayari alikwishasaini mkataba wa miaka miwili
kuifundisha Stars. Burundi ‘Intamba
Murugamba’ itatua nchini Ijumaa tayari kwa
mechi hiyo itakayoshirikisha wachezaji
waliochaguliwa kwenye programu maalumu ya
maboresho ya Stars na wale wakongwe.
Wambura alisema wachezaji 39 wako kwenye
kambi ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam
wakijifua kwa ajili ya mechi hiyo na ile ya Mei
mwaka huu itakayochezwa mkoani Mbeya.
Wachezaji wa Taifa Stars waliopo kambini ni
Deogratias Munishi, Mwadini Ali, Aidan
Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan
Mwasapili, Kelvin Yondani, Said Morad, Amri
Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas
Mkude, Athanas Mdamu, Haruna Chanongo,
Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa,
Ramadhan Singano na Simon Msuva.
Wengine ni Benedicto Mlekwa, Emma
Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba,
Edward Mayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf
Mlipili, Said Ally, Abubakar Mohamed, Hashim
Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito,
Mohammed Saidi, Ayoub Lipati, Abdurahman
Ally na Paul Bundara.
Alitaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni VIP A
Sh 20,000, VIP B na C ni Sh 10,000 na cha
chini ni Sh 5,000.
Tuesday, April 22, 2014
Samata,Ulimwengu na Kazimoto, kuikosa mechi dhidi ya Uganda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment