Friday, April 18, 2014

Azam yatoa ofa,mashabiki wataingia BURE Azam complex kwenye mechi yake na jkt ruvu

UONGOZI wa mabingwa wapya wa soka
Tanzania Bara, Azam FC unatarajia
kutowalipisha kiingilio mashabiki katika
mchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Nassor Idrissa
alisema sababu ya kufanya hivyo ni kuwapa
fursa mashabiki wao kuingia kwa wingi ili
kushuhudia timu yao ikikabidhiwa kombe la
ubingwa huo ambalo wanalitwaa kwa mara ya
kwanza tangu ilipopanda kucheza Ligi Kuu.
“Natarajia kukutana na viongozi wenzangu
halafu tuzungumze na Mwenyekiti wa Bodi ya
Ligi, Silas Mwakibinga tuone kama tunaweza
kuruhusiwa kuwaingiza mashabiki wetu bure
kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya JKT
Ruvu, ili washuhudie timu yao ikikabidhiwa
kombe,” alisema Idrissa.
Idrissa alisema kama yangekuwa mamlaka
yao wenyewe na siyo sheria za Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), wangechukua uamuzi
wa moja kwa moja ya mashabiki kutolipa ili
kuwashukuru kwa sapoti waliyoipa timu yao
tangu mwanzoni mwa msimu hadi siku hiyo ya
mwisho ya kukabidhiwa kombe.
Kwa upande wake, Mwakibinga alisema
endapo Azam FC itataka mashabiki wasilipe
kesho, inatakiwa kukutana na Bodi yake na
kuzungumza ili kujua idadi ya mashabiki
watakaoingia na viingilio vyake.
“Sheria inawaruhusu Azam ila wanachotakiwa
kufanya ni kuja kuonana na viongozi wa Bodi
ya Ligi ili tujadiliane utaratibu tutakao tumia
ikiwemo kujua idadi ya mashabiki
watakaoingia na viingilio ambavyo
vimepangwa kwa ajili ya mchezo huo,” alisema
Mwakibinga.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka
kufahamu idadi kamili ya tiketi ambazo
wataziandaa kwa mchezo huo na mapato
yatakayopatikana ili kufidia garama za
maandalizi zilizofanywa na Bodi hiyo.
Endapo hilo litafanikiwa, Azam FC watabidi
kuilipa Bodi ya Ligi zaidi ya Sh milioni 42
kutokana na kiingilio cha Sh 10,000 kwa
jukwaa kubwa ambalo lina uwezo wa kubeba
watazamaji 150 itaingiza Sh milioni 150 huku
majukwaa mengine ya mzunguko ambayo
kiingilio chake kwa kawaida huwa ni Sh 5,000,
itaingiza Sh 2,750,000. Uwanja una uwezo wa
kuchukua mashabiki 7,000.

No comments:

Post a Comment