Tuesday, April 22, 2014

Simba na Yanga wapigana vikumbo kumsajili kipa wa mtibwa.

SIMBA na Yanga zimeingia kwenye vita moja
ya usajili kwa mara nyingine baada ya kila
mmoja kuhitaji huduma ya kipa wa Mtibwa
Sugar, Hussein Shariff ‘Casillas’, kwa ajili ya
kuvitumikia vikosi vyao kwenye msimu ujao wa
ligi.
Vuguvugu hilo la usajili wa kipa huyo linakuja
baada ya timu zote mbili kuwa na matarajio ya
kupoteza makipa wao, hivyo kila timu inahaha
kutafuta wa kuziba pengo litakaloachwa wazi.
Mtu wa karibu na uongozi wa Simba alilieleza
Championi Jumatano habari hizo kwamba
mpaka sasa kipa aliye kwenye mahesabu ya
miamba yote hiyo miwili nchini ni kipa huyo
ambaye ameonyesha kiwango cha juu msimu
huu .
Chanzo hicho kilisema kwamba Yanga
itampoteza kipa wao, Ally Mustapha ‘Barthez’ ,
baada ya kuugomea uongozi kusaini mkataba
mpya huku Simba ikimpoteza Yaw Berko
ambaye kanuni mpya ya usajili inamtaka
kuondoka nchini kwa kuwa siyo raia wa nchi
hii.
“Berko hataweza kuongezewa mkataba Simba
kutokana na hali ya sheria mpya jinsi ilivyo na
huku Yanga pia Barthez kaugomea uongozi
kusaini mkataba mpya kutokana na vile
alivyosakamwa baada ya mechi ya 3 - 3 na
Simba, kwa hiyo hapo kila timu inahitaji mtu wa
kuziba pengo na ndipo kila mmoja akalitaja jina
la Casillas.
“Lakini sasa hii vita ipo chinichini kwa sababu
Simba hawajui kama Yanga inamtaka Casillas
wala Yanga pia hawajui kama Simba nao
wanamtaka kipa huyo , kwa hiyo kila mmoja
anapita njia yake kuangalia uwezekano wa
kumnasa, ” kilisema chanzo hicho .

No comments:

Post a Comment