KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm,
amesema vijana wake wapo tayari kwa ajili ya
mchezo wa kesho dhidi ya wapinzani wao,
Simba na hana mchezaji yeyote aliyekuwa
majeruhi hadi sasa.
Yanga iliyoingia kambini juzi jioni kwenye Hoteli
ya Bahari Beach, Dar es Salaam ikiwa na
kikosi cha wachezaji 20, imepania kumaliza
msimu vizuri kwa kuifunga Simba ili kupoza
machungu ya kukosa ubingwa uliochukuliwa
na Azam FC katika dakika za mwisho.
“Nina uzoefu na michezo wa watani wa jadi,
huwa inakuwa migumu kwa kila timu kutokana
na kila timu kutaka kuonesha wapenzi,
mashabiki na wanachama wake kuwa wako
vizuri, Simba ni timu nzuri, lakini bado sioni
kikwazo cha kutuzuia tusiibuke na ushindi
katika mchezo huo,” alisema kocha huyo
Mholanzi.
Van Pluijm alisema vijana wake wanazidi
kuonesha mabadiliko makubwa kiuchezaji,
mafunzo yake wanaonekana kuyaelewa vizuri
hivyo kikubwa anaomba waendelee kuwa
katika hali nzuri kuelekea siku ya mchezo na
ana matumaini kitaibuka na ushindi kesho.
“Nina matumaini makubwa sana na wachezaji
waliopo kambini ambao kutokana na mbinu
nilizowapa wanaweza kuwafurahisha
mashabiki wa Yanga na kusahau baadhi ya
watu ambao watakosekana kwenye mchezo
huo,” alisema Van Pluijm.
Wachezaji 20 walioingia kambini kujiandaa na
mechi hiyo ya kesho dhidi ya mahasimu wao,
Simba ni makipa Deogratias Munish “Dida” na
Ally Mustafa “Barthez” kwa upande wa mabeki
ni Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua,
Ibrahim Job, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na
Nadir Haroub “Cannavaro.”
Viungo ni Frank Domayo, Hassan Dilunga,
Salum Telela, Hamis Thabit na Nizar Khalfani
wakati safu ya ushambuliaji wapo Didier
Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Jerson Tegete,
Hamisi Kiza, Hussein Javu na Simon Msuva.
Kocha huyo alisema baada ya kushindwa
kutwaa ubingwa, lengo lake ni kuhakikisha
wanashinda mchezo huo ili kumaliza msimu
huu kwa kuwafunga watani zao Simba ambao
wamekuwa na wakati mgumu msimu huu
kutokana na kushika nafasi ya nne hadi saa.
Friday, April 18, 2014
Pluijm:Tumejipanga kuiadabisha simba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment