Thursday, April 24, 2014

aongezewa mkataba tena au ndio wanamwondoa kimya kimya?

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko
Logarusic amesema amekubaliana
na Zacharia Hanspope na huenda
akabaki Simba.
Logarusic amesema amekutana na
Hanspope ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba na
wamezungumza na kukubaliana.
“Nitabaki Simba kwa makubaliano
yetu hasa kama yatatekelezwa,
nimezungumza na Hanspope,
tumekubaliana.
“Lakini nalazimika kurudi nyumbani
kwanza, nitaondoka kesho asubuhi
kwenda Croatia na baada ya hapo
nitasubiri makubaliano yetu,”
alisema Logarusic.
Alipoulizwa walichokubaliana na
Hanspope ambaye imeelezwa
anatarajia kugombea uenyekiti,
alisema.
“Tumezungumza mambo mengi,
lakini vizuri mkawasiliana naye na
kujua tulichokubaliana. Yeye ndiye
anaweza kuzungumza,” alisema,
kocha wa zamani wa Gor Mahia ya
Kenya.
Mkataba wake ulikuwa ni wa miezi
sita tu baada ya kuichukua Simba
katika mzunguko wa pili.
Pamoja na kuiwezesha kuitwanga
Yanga katika mechi ya Nani Mtani
Jembe, Logarusic alishindwa
kutamba kwenye Ligi Kuu Bara na
kumaliza katika nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment