TIMU ya soka ya Taifa ya Watoto wa Mitaani
ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Kombe la
Dunia kwa Watoto wa Mitaani baada ya juzi
kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa
fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) jana, mshambuliaji Frank
William alifunga mabao matatu katika mechi
hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu
wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi
akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George
Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada
ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo
hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao
4-0.
Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada
ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi
ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania itarejea nchini keshokutwa
ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa
ndege ya shirika la ndege la Muungano wa
Falme za Kiarabu, Emirates.
Tuesday, April 8, 2014
Tanzania bingwa Kombe la DUNIA watoto wa mtaani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment