Tuesday, April 22, 2014

Friends of Simba wamzuia tambwe kwenda Yanga

Tambwe, ambaye hivi karibuni alihusishwa
kutaka kuikimbia klabu hiyo na kwenda
kujiunga na timu nyingine za ligi kuu , amepigwa
pini na klabu hiyo baada ya kuhakikishiwa
neema msimu ujao .
Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe.
Tambwe ambaye ni raia ya Burundi na ambaye
ndiye amekuwa msaada mkubwa wa timu hiyo
msimu huu baada ya kuifungia mabao 19
kweney ligi, amekuwa akihusishwa na taarifa
za kujiunga na Yanga na Azam FC lakini
ameelezwa kuwa kuna kundi moja , Championi
inafahamu kuwa ni Friends of Simba , linaweza
kuingia madarakani na kumtimizia mahitaji
yake yote .
Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage .
Akizungumza na Championi Jumatano ,
Tambwe alisema kuwa hivi karibuni uongozi
wa klabu hiyo umemtaka atulie na asiwe na
haraka za kutaka kuondoka katika kikosi hicho ,
kwani mambo mazuri yanakuja .
Alisema katika mazungumzo aliyofanya hivi
karibuni na Katibu Mkuu wa Simba , Ezekiel
Kamwaga, alimhakikishia kuwa mambo yake
yatakwenda sawa bila tatizo lolote hivyo
anatakiwa kuvumilia mpaka uchaguzi mkuu wa
klabu hiyo utakapomalizika na viongozi wapya
wakipatikana .
“Aliniambia hata kama nikiwa nyumbani
Burundi atakuwa akinijulisha kila kitu
kitakavyokuwa kinaendelea huku , hivyo nisiwe
na wasiwasi mambo yangu yatashughulikiwa,
kwani anaamini uongozi utakaoingia
madarakani, utakuja na mikakati mizuri zaidi
kwa kuwa anaamini wengi wao ni watu wenye
fedha .
“Kutokana na hali hiyo kwa sasa siwezi sema
kama nitaondoka Simba au nitabakia lakini kila
kitu kitajulikana hapo baadaye , acha
niwasikilizie kwanza viongozi hao , nimeelezwa
na mtu mwingine kuwa kuna kundi moja
linatwa Friends lina watu wenye uwezo sana
linaitaka timu nafikiri ni watu ambao
tutawezana,” alisema Tambwe ambaye
mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo
unamalizika mwakani .

No comments:

Post a Comment