KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda anayecheza
Yanga, Haruna Niyonzima amesema hana
presha na kikosi kilichopo kwani ana uhakika
lazima kitoke na ushindi katika mechi dhidi ya
Simba itakayochezwa kesho kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Niyonzima hajacheza mechi tatu za Ligi Kuu
dhidi ya Kagera Suger, JKT Ruvu, Oljoro JKT
na pia kuna uwezekano wa kutocheza mechi
hiyo dhidi ya Simba kutokana na kusumbuliwa
na homa ya matumbo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Niyonzima
alisema kikosi kilichopo kina uwezo wa
kushinda mabao mengi, kwa vile wachezaji
wote ni wakali hata asipokuwapo yeye.
“Ninakiamini kikosi chetu ni kikali, hivyo
lazima tuondoke na ushindi, mimi sitakuwepo
lakini waliopo ni wazuri, watafanya vizuri, na
kuondoka na heshima,” alisema Niyonzima
anayejiuguza nyumbani kwake.
Alisema Simba wamekuwa wakijitapa kwa
maneno kila mwaka, lakini awamu hii Yanga
lazima wawashinde, kutokana na kikosi
kilichopo kucheza kwa kujiamini na juhudi
nyingi hivyo ni rahisi kushinda.
Akizungumzia afya yake, Niyonzima alisema
kwa sasa anaendelea vizuri na hali yake
imeimarika kiasi. Licha ya kuimarika hana
uhakika kama ataendelea kukipiga tena katika
msimu ujao.
“Kwa msimu ujao sifahamu, lakini tusubiri
tutajua, tuombe Mungu tumalize msimu huu
salama,” alisema Niyonzima.
Yanga na Simba zote hazitafuti nafasi ya
kushinda taji kwa sababu tayari bingwa
alishatangazwa toka wiki iliyopita ambao ni
Azam FC isipokuwa kila mmoja anasaka
heshima ili kupunguza utani.
Wakati huo huo, Msemaji wa Yanga, Baraka
Kizuguto alisema tayari wachezaji 20
wameingia kambini juzi kwenye Hoteli ya
Bahari Beach kwa ajili ya maandalizi ya mechi
hiyo ili kuja na nguvu ya kusaka ushindi.
Friday, April 18, 2014
Niyonzima: Ushindi lazima dhidi ya simba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment