HOMA ya michezo miwili ya Kundi C Ligi
Daraja la Kwanza Tanzania Bara itakayoamua
timu moja kati ya mbili za Mkoa wa Shinyanga
zinazochuana kuwania kushiriki katika Ligi Kuu
Tanzania Bara msimu ujao, Standa United na
Mwadui FC imezidi kupanda kuelekea mechi za
kesho.
Stand United na timu iliyoshuka daraja msimu
uliopita ya Toto African ya Mwanza zitakwaa
kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini
hapa wakati pambano jingine litafanyika
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kati
ya Polisi Dodoma watakapoikaribisha Mwadui
FC.
Tambo na majigambo ya mashabiki wa timu
hizo mbili yametawala anga la Mkoa wa
Shinyanga kwa wapenzi kutambiana nani
ataibuka mshindi kesho ili kuingia Ligi Kuu
msimu ujao huku kila mmoja akitamba kuwa
timu yake itashinda kwa kishindo.
Kesho ni siku ya mwisho kwa michezo ya
Kundi C kwa timu zote nane kuteremka
dimbani kuwania pointi tatu muhimu huku
Mwadui ikiwa kileleni baada ya kujikusanyia
pointi 28 ikifuatiwa na ndugu zao wa Stand
United yenye pointi 26, Toto African ikiwa na
pointi 21 na JKT Kanembwa ya Kigoma wakiwa
na pointi 20.
Akizungumza na gazeti hili, mpenzi wa soka
mkoani hapa, Ally Nassoro wa Maganzo
alisema ana uhakika wa asilimia 100 kuwa
nafasi kubwa ya kuingia kwenye Ligi Kuu iko
kwa Mwadui kwa kuwa ina pointi 28 hata
ikitoka sare itafikisha pointi 29 na itakuwa na
nafasi kubwa zaidi ya kuizidi idadi ya mabao
Stand United ambayo ikishinda mchezo wake
dhidi ya Toto itafikisha pointi 29 sawa na
Mwadui.
Mpenzi mwingine, Ndimila Jilala wa Ngokolo
katika Manispaa ya Shinyanga alisema ushindi
wa Stand United uko dhahiri kwa kuwa pamoja
na ushindi kesho, bado inategemea rufaa yake
iliyokata Shirikisho la Soka (TFF), dhidi ya JKT
Kanembwa kwa kuwachezesha wachezaji
iliowasajili kwenye dirisha dogo kinyume cha
maelekezo ya TTF katika mchezo ambao
ilishinda bao 1-0.
Jilala alishangazwa na ukimya wa TFF
kuchelewesha kutoa maamuzi ya rufaa hiyo
mpaka sasa ligi inakaribia kufikia tamati, jambo
linalotia wasiwasi ni kwa nini rufaa hiyo
imechelewa kiasi hicho.
Timu nyingine za Kundi C ambazo tayari
zimepoteza matumaini ya kuingia Ligi Kuu
kutokana na uchache wa pointi ni Polisi
Tabora yenye pointi 17, Polisi Mara pointi 12,
Polisi Dodoma pointi 11 na Pamba pointi nane.
Friday, April 4, 2014
Nani kufuzu kuingia ligi kuu tanzania bara ??? Stand utd Vs Mwadui
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment