**Mzungu wa Yanga atinga mazoezini na jezi Nyekundu**
KATIKA hali ya kustaajabisha, Kocha Mkuu wa
Yanga, Hans van Der Pluijm, juzi alileta
sintofahamu baada ya kutinga mazoezini na
jezi yenye logo ya doti jekundu, ambayo ni
‘nuksi ’ Jangwani.
Mazoezi hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa
Ununio, wakijifua kwa ajili ya mtanange wa
heshima dhidi ya watani wao Simba,
utakaopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa Dar .
Mholanzi huyo alikuwa ametinga ‘full ’ jezi
nyeusi ya Klabu ya Feyenoord Rotterdam ya
nchini Uholanzi , inayotumia logo yenye doti
jekundu na nyeupe, ambayo ni kinyume na
miiko ya Yanga .
Ikumbukwe kuwa Yanga waliingia katika
mgogoro mkubwa na wadhamini wa Ligi Kuu
Bara, kampuni ya Vodacom , wakikataa kutumia
logo yenye doti jekundu kwa kile kilichoelezwa
na Baraza la Wazee kupitia katibu wao, Ibrahim
Akilimali, kuwa ni nuksi na kuongeza kuwa
katiba yao imeeleza kukataa rangi nyekundu
Jangwani.
Championi ilikuwa shuhuda katika mazoezi ya
Yanga, ambapo Mholanzi huyo hakuonekana
kujali, pengine hofu ikatawala labda wazee
hawajampa utaratibu na miiko ya klabu hiyo .
Feyenoord, ni moja ya timu zenye jina kubwa
nchini Uholanzi , ambayo mastaa wakubwa
akiwemo straika wa Manchester United , Robin
Van Persie, walipitia.
**CCTV kufungwa uwanjani**
KATIKA kuhakikisha ulinzi na usalama
unapatikana katika mechi ya leo Jumamosi kati
ya Yanga na Simba kwenye Uwanja wa Taifa,
jumla ya askari 400 wameandaliwa kwa ajili ya
kuweka usalama huku kukiwa na magari
mawili ya wagonjwa, yaani wale ambao
watazimia au kupata matatizo uwanjani hapo.
Mchezo huo wa watani wa jadi utapigwa leo
katika Uwanja wa Taifa ukiwa ni moja ya mechi
za kufungia msimu wa 2013/ 2014 ambapo
katika mchezo huo , mshindi wa pili ambaye ni
Yanga atakabidhiwa zawadi ya medali .
Akizungumza na Championi Jumamosi ,
Mtendaji wa Bodi ya Ligi , Silas Mwakibinga,
alisema wameandaa askari 400 na ‘Ambulance ’
mbili kwa ajili ya mchezo wa Simba na Yanga
huku ulinzi na usalama ukiwa wa hali ya juu .
Mwakibinga alisema kuwa wamejiandaa vyema
kabisa na michezo ya kufunga ligi kuu ambayo
yote itachezwa kesho katika viwanja
mbalimbali huku bingwa na mshindi wa pili
wakikabidhiwa zawadi zao kesho.
“Tumeandaa askari 400 kwa ajili ya usalama
katika mechi ya Simba na Yanga na ulinzi kwa
jumla umeimarishwa kila kona huku magari ya
kubebea wagonjwa tumeandaa mawili kwa
lolote litakalojitokeza .
“Kwa upande wa watu wa uwanja, wao
wamefunga ‘security ‘ kamera ( CCTV ) pale kwa
usalama zaidi na hiyo ni ya moja kwa moja si
kwa mchezo pekee wa kesho ( leo) , hivyo kila
kitu kinakwenda safi .
“Lakini kwa bingwa , atakabidhiwa zawadi yake
Chamazi ambazo ni kombe na medali za
dhahabu huku mshindi wa pili taifa yeye
atapewa medali zake pia ,” alisema
Mwakibinga.
**Friends of simba wamteka Okwi**
SAA chache kabla ya mechi ya watani , Yanga
dhidi ya Simba, kama kawaida vituko vinazidi
kuongezeka na mshambuliaji Emmanuel Okwi
anazidi kuwa tatizo .
Okwi alikuwa acheze mechi ya leo , akasusa
kwa kuwa anawadai Yanga dola 40,000 (Sh
milioni 64 ), lakini sasa Friends of Simba
wameingilia na kumteka mawazo zaidi kuwa
hana haja ya kucheza mechi ya leo ,
ataangushiwa mzigo wakipoteza.
Rafiki wa karibu wa Okwi amesema mara
nyingi mchezaji huyo amekuwa akijichimbia
katika hoteli anayoishi na hivi karibuni
alizungumza na memba wa kundi la Friends of
Simba linaloaminika kwa mipango ya kisoka na
kupewa ushauri kwamba hana sababu ya
kucheza mechi hiyo.
“Awali Okwi alikuwa apewe dola 20,000
ambazo ni nusu ya zile anazodai ili acheze ,
lakini baadaye mambo yakabadilika, ninafikiri
ametekwa mawazo na wale Friends of Simba.
“Unajua Friends wamerudi Simba, wanataka
kukiimarisha kikosi chao na ndiyo wametoa
msaada kuipeleka Simba Zanzibar na mmoja
wa mabosi wao ( Zacharia) Hans Pope ndiye
amelipa mshahara wa wachezaji wote maana
waligoma,” kilieleza chanzo kutoka Yanga .
“Kwa fitna wanajulikana , wameamua kupigilia
msumari Okwi asicheze kabisa. Wanajua
Simba haipati kitu lakini wanachotaka ni Simba
kutopoteza. ”
Juhudi za kumpata Okwi hazikuzaa matunda
kutokana na simu yake kupigwa zaidi ya mara
mbili bila ya majibu . Lakini memba mmoja wa
Friends of Simba kasisitiza kweli
walizungumza na Okwi lakini kwa lengo la
kumpa pole tu.
“Mimi si msemaji wa Friends of Simba, lakini
Okwi ni kijana wetu na tumezungumza naye
kumpa pole kutokana na matatizo ya fedha
anazodai na hajalipwa hadi leo , ubaya ni upi ?
“Msisahau, sisi ni ndugu zake na ndiyo
tulimleta Tanzania . Sasa hatuwezi kuwa
maadui, pia akipata matatizo tunaweza
kuzungumza naye au kumshauri tu,” alisema
akisisitiza kutoandikwa .
Mechi ya leo haiwezi kuzipa Yanga wala Simba
mabadiliko kwenye msimamo lakini ina nguvu
ya mechi ya watani , kila upande unataka
kushinda.
Wakati huohuo , Kocha Mkuu wa Yanga, Hans
van Der Pluijm, amefunguka na kusema
kamwe hafanyi kazi kwa kutegemea wachezaji
fulani wenye majina.
Van Der Pluijm amesema: “ Siku zote sifanyi
kazi kuangalia nani hayupo kikosini, labda
anaweza kutugharimu, nafanya kazi kwa
kuangalia nani ananifaa kikosini.
“Kazi yangu ni kuangalia kikosi nilichonacho
kinafanya vema kuelekea mchezo fulani , basi ,”
alisema kocha huyo wa zamani wa Feyenoord
ya Uholanzi .
Yanga itawavaa Simba leo bila nyota wengi,
wakiwemo Okwi mwenye mgomo baridi , Juma
Kaseja ( matatizo binafsi) , Juma Abdul (kadi
tatu za njano ) , Haruna Niyonzima, Said
Bahanuzi (wanaumwa) .
**Dida:Tambwe leo hapati goli ng'oo**
KIPA namba moja wa Yanga, Deogratius
Munishi ‘Dida ’, ameeleza kuwa katika mchezo
wa leo dhidi ya Simba, atahakikisha
mshambuliaji Amissi Tambwe hapati bao .
Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe.
Dida anatarajiwa kukaa langoni leo katika
mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu
huu dhidi ya watani wao wa jadi Simba kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar .
Akizungumza na Championi Jumamosi , Dida
alisema atawapanga vizuri mabeki wake
kuhakikisha Tambwe hafungi bao lolote hata la
kuotea.
“Ninajua mchezo utakuwa mgumu lakini nina
imani mabeki wangu watanilinda vizuri na
kuhakikisha wanazuia kikamilifu mashambulizi
ya Simba na kutotoa nafasi kwa Tambwe
kufunga bao lolote .
No comments:
Post a Comment