TIMU ya soka ya Mbeya City ya hapa,
imekanusha tuhuma zinazotolewa dhidi yake
za kula njama za kuiwezesha Azam FC
kushinda katika mchezo wa kesho ili timu hiyo
inyakue ubingwa wa Tanzania bara.
Tuhuma zinazotajwa dhidi ya timu hiyo ni
kuahidiwa na Azam kununuliwa basi la kisasa
kwa ajili ya timu na pia Kocha Mkuu Juma
Mwambusi kununuliwa nyumba eneo la
Chamazi jijini Dar es Salaam ili apange kikosi
chenye wachezaji dhaifu siku ya mchezo.
Zipo tuhuma pia za wachezaji wa kikosi cha
kwanza kupewa rushwa ili siku ya mchezo huo
kwenye Uwanja wa Sokoine, wacheze chini ya
kiwango na kuipa ushindi Azam FC ili itangaze
ubingwa.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari na Katibu wa Mbeya City, Emmanuel
Kimbe, imebainishwa kuwa tuhuma hizo si za
kweli na timu hiyo inaamini kuwa tuhuma
zinaibuliwa na watu wachache wasiopenda
mafanikio ya timu hiyo iliyobahatika kujizolea
mashabiki lukuki ndani na nje ya Mkoa wa
Mbeya tangu kutinga kwake Ligi Kuu ya
Tanzania Bara msimu huu.
Kimbe aliyezitaja tuhuma hizo sawa na
propaganda na upotoshaji, alisema mpango wa
Halmashauri ya Jiji la Mbeya kununua basi la
timu zake za soka na netiboli ambazo zote
ziko Ligi Kuu za michezo husika.
“Halmashauri ya jiji la Mbeya imekuwa katika
mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa
ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri,
ikiwemo kutumiwa na timu zake (netiboli na
mpira wa miguu) ambazo zote zipo Ligi Kuu ya
michezo husika kwa kufuata sheria ya
manunuzi ya umma,” alisema Kimbe.
Alisema mchakato huo ulianza Agosti 8, 2013,
kwa kutangaza zabuni baada ya kutenga bajeti
katika mwaka wa fedha 2012/13 na 2013/14,
na kwamba hawakupata mzabuni mwenye
sifa, hivyo tangazo hilo lilirudiwa kutangazwa
tena Februari 12, mwak huu.
Alisema pamoja na mchakato huo, pia klabu
inaendelea na mazungumzo na wadau
mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa
udhamini wa bidhaa zao, moja ya maeneo ya
udhamini ni ununuzi wa basi la wachezaji
taratibu na makubaliano haya
yatakapokamilika wapenzi wa soka
watajulishwa, hivyo tuhuma za kuahidiwa
kununuliwa basi, zinalenga kuidhalilisha timu
hiyo.
Kuhusu tuhuma kwa kocha Mwambusi
kununuliwa nyumba Chamazi ili apange kikosi
dhaifu kesho, Kimbe alisema kocha huyo ni
mwajiriwa wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya,
kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo
amekuwa na timu hiyo kwa muda mrefu sasa
na ataendelea kuwepo.
Alisema kumekuwepo na maneno yasiyofaa
dhidi ya Mwambusi tangu mzunguko wa pili wa
ligi kuanza, aliyosema yamekuwa na nia ya
kuharibu mwenendo wa timu ili ianze kufanya
vibaya, lakini zaidi ya hapo yana nia ya
kumdhalilisha kocha na taaluma ya ukocha
nchini.
Katibu huyo aliwapongeza pia wachezaji wa
Mbeya City, akisema ndiyo wachezaji wenye
nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu ndani
na nje ya uwanja, kwani ni waadilifu na
wanajua wanataka nini.
Mbeya City ambayo inashika nafasi ya tatu
katika msimamo wa Ligi Kuu, kesho
inaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa
Sokoine katika mechi ambayo timu ya Chamazi
ikishinda, itatangazwa bingwa.
Friday, April 11, 2014
Mbeya city: hatujaongwa na azam ili tuhujumu mechi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment