KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema Azam FC ishindwe yenyewe
kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara,
kwa sababu ana uhakika wa kuifunga Yanga
kwenye mchezo wa mwisho wa ligi hiyo Aprili
19, mwaka huu.
Logarusic, ambaye kikosi chake hakina uwezo
hata wakumaliza ligi ya msimu huu kwenye
nafasi ya tatu, alisema anachotaka ni
kuendeleza rekodi yake ya kuifunga Yanga
kwa sababu ndiyo timu pekee yenye ushindani
na kikosi chake tofauti na Azam.
“Ni kweli hatuna uwezo hata wa kumaliza
nafasi ya tatu na hiyo ndiyo itakuwa mechi yetu
ya mwisho kwenye msimu, tumepanga
kuwavurugia Yanga kwa kuwafunga na
kuwapa furaha mashabiki wetu ambao msimu
huu umekuwa mbaya kwao,” alisema
Logarusic.
Kocha huyo raia wa Croatia, alisema pamoja
na upungufu uliopo kwenye kikosi chake
ukilinganisha na kile cha Yanga, hawatakubali
kufungwa na kuwafanya wapinzani wao
walipize kisasi cha mabao 3-1, ambacho
waliwapa kwenye mechi ya Mtani Jembe
Desemba 21, mwaka jana.
“Najua Yanga wana timu nzuri, lakini Azam ni
zaidi yao na ndiyo timu ninayoipa nafasi kubwa
ya kuchukua ubingwa kutokana na ukali wa
kikosi walichokuwa nacho ambacho sidhani
kama kinaweza kikafanya mzaha,” alisema
Logarusic.
Wednesday, April 9, 2014
Logarusic (kocha wa simba) aipa nafasi azam kuchukua ubingwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment