TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars jana
ilifanikiwa kufuzu raundi ya pili ya kuwania
kufuzu fainali za kombe la Mataifa Afrika
baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na
Zimbabwe katika mchezo mkali wa marudiano
uliofanyika jijini Harare.
Kwa matokeo hayo Stars imefuzu kwa ushindi
wa jumla ya mabao 3-2 baada ya kushinda
bao 1-0 katika mechi ya awali iliyofanyika Dar
es Salaam wiki mbili zilizopita kwa bao
lililofungwa na John Bocco dakika ya 36. Stars
sasa itacheza na msumbiji iliyoitoa Sudani
Kusini kwa jumla ya mabao 5-0.
Kwa mujibu wa blog ya
bongostaz.blogspot.com Zimbabwe ndiyo
waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza
katika dakika ya tatu ya mchezo lililofungwa na
Danny Phiri kufuatia shambulizi kubwa kwenye
lango la Stars na kujipatia bao hilo ambalo
lilifufua matumaini ya Wazimbabwe kusonga
mbele.
Hali iliwabadilikia ghafla Wazimbabwe baada ya
Nahodha wa Stars Nadir Haroub
kuisawazishia Tanzania bao hilo kwa kichwa
akiunganisha kona ya Simon Msuva dakika ya
21 na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1 hadi
mapumziko.
Kipindi cha pili Stars iliyo chini ya kocha
Mholanzi Mart Nooij, ilikianza kwa kasi na
kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya
46 lililofungwa na Thomas Ulimwengu baada
ya mabeki wa Zimbabwe kudhani ameotea.
Hata hivyo bao hilo la Stars halikudumu kwani
dakika ya 54 wenyeji Zimbabwe,
walisawazisha kupitia kwa Denver Mukamba,
aliyepiga kona iliyoingia moja kwa moja
wavuni.
Bao hilo liliibua ari ya wachezaji wa na kuanza
kucheza kwa kasi na kulisakama lango la
Stars kwa muda mrefu lakini ngome imara
iliyokuwa chini ya Nahodha Haroub kipa
Deogratius Munish na Said Morad aliyeingia
kipindi cha pili ilikuwa makini kwa kuondosha
hatari zote zilizoelekezwa langoni mwao.
Baada ya kuona timu yake inaelemewa zaidi
dakika za mwishoni kocha Nooij aliwatoa
Msuva na Ulimwengu nafasi zao
zikachukuliwa na Moradi pamoja na Mrisho
Ngassa ambao waliongeza uimara na
kufanikiwa kulinda matokeo yasibadilike.
Monday, June 2, 2014
Taifa stars iyoooooooo....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment