Polisi katika mjini wa São Paulo nchini Brazil
wametumia mabomu ya machozi kutawanya
waandamanaji wanaopinga Kombe la Dunia, ikiwa
ni saa chache tu kabla ya michuano hiyo kuanza.
Taarifa zinasema mtu mmoja amekamatwa na
mwandishi mmoja wa CNN kujeruhiwa.
Waandamanaji wanasema wamepanga
kuandamana karibu na uwanja ambao shughuli ya
ufunguzi itafanyika.
Maandamano zaidi yamepangwa katika miji
mingine ya Brazil kupinga michuano hiyo
kuandaliwa nchini humo.
Picha za TV kutoka São Paulo zinaonesha polisi
wa kutuliza ghasia wakitumia mabomu ya
machozi na risasi za mpira karibu na uwanja wa
Corinthians.
Waandamanaji hao wamekuwa wakiimba-
wakisema "hakutakuwa na kombe hapa".
Thursday, June 12, 2014
MABOMU YARINDIMA MJI WA SAO PAULO .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment