Saturday, February 15, 2014

SUPER SUB: Mabao 132 yamefungwa Ligi Kuu England na nyota walioanzia benchi

YANAPOTAJWA majina yao; David Fairclough,
Ole Gunnar Solskjaer, Tore Andre Flo na hawa
wa siku za hivi karibuni akina Edin Dzeko na
Javier Hernandez, kitu cha kwanza kinachokuja
akilini ni kwamba hao ni wakali wa kubadili
matokeo ya mchezo wa soka wanaoanzia
kwenye benchi.
Kwenye mchezo wa soka kuna lugha yake
inayowatambulisha watu hawa ‘Super Sub’.
Wachezaji wanaoanzishwa benchi kwenye
mechi kadhaa na kisha kila wanapoingizwa
husababisha matokeo ya mchezo kubadilika
kwa maana ya kufunga mabao au kutengeneza
mabao hayo, nyota hawa hutambulika kwa jina
la ‘Super Sub’.
Kwenye Ligi Kuu England, klabu za Manchester
City, Swansea na West Bromwich Albion,
zimewatumia sana wachezaji hao na kuvuna
mabao 12 ambayo yamewasaidia katika kupata
matokeo bora kwenye mechi zao.
Lakini, katika mikikimikiki ya ligi hiyo, kuna
timu ambayo imechemsha na kushindwa kupata
hata bao moja licha ya kufanya mabadiliko
mengi zaidi ya wachezaji kuliko klabu nyingine
zote kwenye Ligi Kuu England.
Norwich City ambayo kocha wake, Chris
Hughton, amebadilisha wachezaji mara 63,
lakini hakuna hata mmoja kati ya nyota wake
walioanzia benchi aliyeweza kufunga mabao au
kusababisha bao kufungwa.
Hadi kufikia sasa kwenye msimu huu, kwenye
matokeo ambayo timu yake imefungwa,
Hughton alifanya mabadiliko 63 ya wachezaji
akiwa na imani ya kubadili matokeo, lakini
hakufanikiwa.
Wachezaji walioanzishwa benchi na kisha
kuingizwa uwanjani ili wakabadili matokeo,
lakini wakashindwa kufanya hivyo ni pamoja na
Robert Snodgrass, Wes Hoolahan, Johan
Elmander, Jonny Howson, Anthony Pilkington,
Alexander Tettey, Ryan Bennett, Gary Hooper,
Nathan Redmond, Josh Murphy, Steven
Whittaker, Ricky van Wolfswinkel, Luciano
Becchio na Leroy Fer.
Kwenye Ligi Kuu England wakati kwa sasa
upinzani zaidi ukiwa umeongezeka kwenye
nafasi nne za juu, katikati na mkiani, kuna timu
zimefaidika na wachezaji wanaoanzia benchi
kutokana na kusababisha matokeo mazuri kila
wanapoingizwa.
Kwenye Top Four
Manchester City inashika nafasi ya tatu kwenye
msimamo wa Ligi Kuu England na pointi zake
54, tatu nyuma ya vinara Chelsea. Lakini kikosi
hicho kinachonolewa na Manuel Pellegrini,
kimevuna mabao mengi zaidi yaliyotokana na
wachezaji wake walioanzia benchi.

No comments:

Post a Comment