TIMU ya Mbeya City ya Mbeya, ipo kwenye
mchakato wa ujenzi wa uwanja wao na
kushusha nchini kontena moja la jezi zao
kutoka nchini China.
Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu, kama
ikifanikiwa kutimiza yote hayo basi
kimaendeleao itazizidi klabu kongwe za Simba
na Yanga ambazo hadi sasa hazina hata viwanja
vya maana vya mazoezi.
Akizungumza na Mwanaspoti, mwenyekiti wa
timu hiyo, Mussa Mapunda alisema kuwa tayari
wamenunua shamba la ekari 15 eneo la
Iwambi, Mbeya ambalo wamelitenga kwa ajili
ya kujenga uwanja mkubwa wa kisasa.
Alisema, tofauti na uwanja wamepanga kujenga
hosteli za kisasa watakazozitumia wachezaji wa
timu kubwa, pia kwa ajili ya timu zao za vijana
kuanzia umri chini ya miaka 14 hadi 20
watakaowatumia siku zijazo.
Pia watatenga eneo lingine kwenye uwanja huo
kwa ajili ya kituo cha michezo. Timu hiyo kwa
sasa inatumia Uwanja wa Sokoine unaomilikiwa
na CCM.
Akifafanua kuhusu kuingiza nchini kontena
moja la vifaa vya michezo kutoka China ambalo
litakuwa na jezi, suti za michezo, kofia, skafu,
bendera na soksi. Vitu hivyo vitauzwa nchini
kote pamoja na nchi za Malawi na Zambia.
Tuesday, February 18, 2014
Mbeya City waanza mchakato wa ujenzi wa uwanja wao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment