Wednesday, May 14, 2014

Angalia hapa mpira utakaotumika kwenye mechi za kombe la dunia

Je kifaa hiki kitaweza? Hilo ndilo swali linaloulizwa
na wengi kuhusu Brazuca, jina la mpira rasmi
utakaotumiwa katika dimba la Kombe la Dunia
lijulikanalo kama Brazil 2014.
Mpira huo ni wa 12 kuundwa na kampuni ya Adidas
kwa kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia.
Kampuni hiyo ilikosolewa miaka minne iliyopita juu
ya mpira uliojulikana kama Jabulani, mpira rasmi
wa Kombe la Dunia wa mwaka 2010 Afrika Kusini.
"hauna mwelekeo angani na hautabiriki," ndivyo
alivyosema mlinda lango wa Italia Gianluigi Buffon,
naye mshambulizi wa Brazil Luis Fabiano alisema
mpiro huo ulikuwa wa "kimiujiza".
Adidas sasa inadai kuwa Brazuca imeimarisha
mguzo wake na shabaha.
" Tumefanya uchunguzi unaohusiana na mwendo
wa mpira huu na matokeo yanaonyesha kuwa
unasafiri na kupaa kwa njia zinazotarajiwa na
kujipinda kokote ni kudogo sana hivi kwamba
hakutambuliki," mkurugenzi wa kandanda wa
Adidas Matthias Mecking aliambia BBC.
Wataalamu wa kasi angani waliohojiwa na BBC
walisema kuwa kuna sababu tatu zitakazotumiwa
kuamua matumizi ya mpira wa Kombea la Dunia la
Brazil 2014.
"jambo muhimu sana kwa mpira huo ni jinsi ulivyo
"Kitu muhimu sana kuhusu mpira ni mguso wake,''
alieleza Daktari Rabi Mehta, afisa mkuu katika kituo
cha utafiti wa mambo ya anga za juu nchini
Marekani.
Daktari Rabi Mehta, aliambia BBC kuwa amefanya
majaribio ya mpira ya Jabulani katika shimbo lenye
hewa na amekuwa akichunguza Brazuca nao.
Anasema kuwa hali ya kukosa mwelekeo hutokea
wakati mpira hauzunguki au ukizunguka polepole
sana.
Mehta anasema mpira ulipokua laini unapopaa
kwenye anga bila kuzunguka, hewa iliyo karibu nao
inaingilia maeneo ambako ngozi inakutana na
kusabisha mpira kupata mwelekeo tofauti.
Ingawa mshambulizi matata wa Brazil Luis Fabiano
(kushoto) ameutaja huo mpira wa 2010 kama wa
kimiujiza lakini Daktari Mehta anasema kwa
kufanya mpira huo usiwe laini ni kama "tumerejea
tulikokuwa."
Baadhi ya wachezaji waliwahi kulalamika kuhusu
mpira wa Jabulani uliotumiwa Afrika Kusini
Mipira isiyo laini husafiri mwendo mrefu zaidi. Mpira
unapopaa hewani, huchochea na kusukuma hewa,
jinsi mashimo madogo yaliyoko kwenye mpira wa
gofu, Daktari Simon Choppin anasema.
"Hali hiyo ya kuchochea ni muhimu kwa kasi na
mwendo wa kutegemewa. Mpira ulio laini kabisa
hukabiliana na upepo mwingi na kuvuruga mwendo
wa hewa, " Bwana Choppin anasema.
Je uamuzi wa wanasayansi ni upi?
"nina hakika kuwa Brazuca utakuwa na tabia sawa
na ule wa asili ulio na vipande 32 vilivyoshonwa
kama hapo awali kwa hivyo malalamiko kama yale
tuliyotolewa katika mashindano mawili yaliyopita ya
Kombe la Dunia yatapunguka," Rabi Mehta alisema.

No comments:

Post a Comment